Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • “Aliporudiwa na fahamu zake, alisema, ‘Ni wanaume wangapi walioajiriwa wa baba yangu ambao wanazidi katika kuwa na mkate, na huku mimi ninaangamia hapa kutokana na njaa kali!

  • “Yehova, Mungu Mwenye Rehema na Neema”
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Oktoba 1
    • 13 Mwana mpotevu ‘alirudiwa na fahamu zake.’ Kwa muda, mwana mpotevu alikuwa amejiingiza katika kutafuta anasa, kana kwamba alikuwa katika ulimwengu usio halisi. Lakini sasa alifahamu kabisa hali yake halisi ya kiroho. Ndiyo, hata ingawa alikuwa amejikwaa, bado kulikuwa na tumaini kwa mwanamume huyu kijana. Alikuwa na sifa fulani nzuri. (Mithali 24:16; linganisha 2 Mambo ya Nyakati 19:2, 3.) Namna gani wale wanaoliacha kundi la Mungu leo? Je, lingekuwa jambo lenye kupatana na akili kukata kauli kwamba, wote hao hawana tumaini kabisa, kwamba kwa vyovyote mwendo wao wa kuasi wathibitisha kwamba wamefanya dhambi dhidi ya roho takatifu ya Mungu? (Mathayo 12:31, 32) Si lazima iwe hivyo. Baadhi yao huumizwa sana na mwendo wao mkaidi, na hatimaye wengi wao hurudiwa na fahamu zao. “Sikumsahau Yehova kamwe, hata siku moja,” asema dada mmoja, akikumbuka muda aliokaa nje ya tengenezo la Mungu. “Sikuzote nilisali kwamba kwa njia fulani, siku moja angenikubali niirudie kweli.”—Zaburi 119:176.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki