-
Matukio Yaliyotabiriwa Kuhusu Siku ZetuMnara wa Mlinzi—2008 | Oktoba 1
-
-
Matetemeko Makubwa ya Nchi. Yesu alisema: “Kutakuwa na matetemeko makubwa ya nchi.” (Luka 21:11) Ikiwa unaona kwamba siku hizi watu wengi zaidi kuliko wakati mwingine wowote wanaathiriwa na matetemeko ya nchi, hujakosea. Mtaalamu Mhindi wa matetemeko ya nchi, R. K. Chadha, alisema hivi mnamo 2007: “Kwa ghafula, tunaona ongezeko la utendaji chini ya ardhi unaosababisha matetemeko ulimwenguni pote. . . . Hakuna mtu anayejua sababu.” Zaidi ya hayo, kuongezeka kwa watu katika maeneo yanayokumbwa na matetemeko ya nchi kumeongeza idadi ya wale wanaoathiriwa na misiba hiyo. Tetemeko lililokumba Bahari ya Hindi mnamo 2004 na tsunami iliyofuata ilifanya mwaka huo kuwa “na matetemeko hatari zaidi kwa miaka 500 hivi” na “wa pili hatari zaidi kuwahi kurekodiwa,” kulingana na Shirika la Marekani la Uchunguzi wa Jiolojia.
-
-
Matukio Yaliyotabiriwa Kuhusu Siku ZetuMnara wa Mlinzi—2008 | Oktoba 1
-
-
Magonjwa Yasiyoweza Kuzuiwa. “Kutakuwa na tauni,” Yesu alitabiri. (Luka 21:11) Ulimwenguni pote, magonjwa ya zamani na mapya yanawapata watu wengi zaidi, na ni vigumu kuyatibu. Kwa mfano, muda wa kufikia miradi ya kimataifa ya kumaliza malaria umehitaji kusogezwa mbele mara kadhaa kwa kuwa ugonjwa huo unaendelea kuwashinda wanadamu. Kwa kuongezea, mamilioni wanakufa kwa sababu ya magonjwa ya zamani, kutia ndani kifua kikuu (TB), UKIMWI, na magonjwa mengine mapya. “Asilimia 33 hivi ya watu ulimwenguni wameambukizwa TB,” linaripoti Shirika la Afya Ulimwenguni. Shirika hilo pia linasema kwamba virusi vya UKIMWI vinachangia kuongezeka kwa TB katika nchi nyingi. Kila sekunde, kuna mtu anayeambukizwa TB, na ugonjwa huo unazidi kushinda madawa nguvu. Mnamo 2007 mgonjwa huko Ulaya aliambukizwa TB ambayo “ilishinda madawa yote tuliyo nayo,” linaripoti gazeti moja (New Scientist).
-