Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Februari 1
    • Miezi sita tu baada ya Yesu kuanza huduma yake duniani, Nikodemo anamtambua ‘kuwa mwalimu kutoka kwa Mungu.’ Kwa kuvutiwa na miujiza ambayo Yesu alikuwa amefanya karibuni huko Yerusalemu kwenye Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka wa 30 W.K., Nikodemo anakuja usiku kukiri kwamba anamwamini Yesu na pia kujifunza mengi zaidi kuhusu mwalimu huyo.

  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Februari 1
    • Yohana 3:1-

  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Februari 1
    • Pia ana ufahamu mwingi kwa kuwa anaweza kutambua kwamba Yesu ni mwalimu aliyetumwa na Mungu. Nikodemo anapendezwa na mambo ya kiroho, na ni mnyenyekevu isivyo kawaida. Ni jambo gumu kama nini kwa mshiriki wa mahakama kuu zaidi ya Wayahudi kukiri kwamba mwana wa seremala tu ni mtu aliyetumwa na Mungu!

  • Jifunze Kutoka kwa Nikodemo
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Februari 1
    • Kwanza kabisa, Yohana anasema kwamba mtawala huyo wa Wayahudi “alimjia [Yesu] wakati wa usiku.” (Yohana 3:2) Msomi mmoja wa Biblia anadokeza: “Nikodemo alikuja usiku si kwa sababu aliogopa, bali kwa sababu alitaka kuepuka umati ambao ungekatiza mazungumzo yake pamoja na Yesu.” Hata hivyo, Yohana anamtaja Nikodemo kuwa “yule mtu aliyemjia [Yesu] usiku mara ya kwanza” na katika muktadha huohuo anamtaja Yosefu wa Arimathea kuwa “mwanafunzi wa Yesu lakini wa siri kutokana na kuhofu kwake Wayahudi.” (Yohana 19:38, 39) Kwa hiyo, inaelekea kwamba Nikodemo alimjia Yesu usiku kwa ‘kuhofu Wayahudi,’ kama vile wengine walioishi wakati huo walivyohofu kuhusianishwa na Yesu.—Yohana 7:13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki