Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Wafarijini Watu Wangu’
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Isaya aandika: “Sikiliza, ni sauti ya mtu aliaye, Itengenezeni nyikani njia ya BWANA [“Yehova,” “NW”]; nyosheni jangwani njia kuu kwa Mungu wetu. Kila bonde litainuliwa, na kila mlima na kilima kitashushwa; palipopotoka patakuwa pamenyoka, na palipoparuza patasawazishwa; na utukufu wa BWANA utafunuliwa, na wote wenye mwili watauona pamoja; kwa kuwa kinywa cha BWANA kimenena haya.”—Isaya 40:3-5.

      6 Kabla ya kuanza safari, mara nyingi watawala wa Mashariki wangetuma watu kuitengeneza njia kwa kuondoa mawe makubwa na hata kujenga madaraja na kusawazisha vilima. Kwa Wayahudi wanaorudi, itakuwa kana kwamba Mungu mwenyewe yuko mstari wa mbele, akiondoa vikwazo vyovyote vile. Kwani, hao ni watu wa jina la Yehova, na kutimiza ahadi yake ya kuwarudisha nchini kwao kutafanya utukufu wake udhihirike mbele ya mataifa yote. Yapende yasipende, mataifa hayo yatalazimika kutambua kwamba Yehova ndiye Mtimizaji wa ahadi zake.

      7, 8. (a) Maneno ya Isaya 40:3 yalitimiaje katika karne ya kwanza W.K.? (b) Unabii wa Isaya ulitimiaje kwa njia kubwa zaidi mwaka wa 1919?

      7 Kurudishwa kulikotukia karne ya sita K.W.K. hakukuwa ndio utimizo pekee wa unabii huo. Kulikuwapo pia utimizo fulani katika karne ya kwanza W.K. Yohana Mbatizaji alikuwa ndiye sauti ya mtu ‘apaazaye kilio nyikani,’ akitimiza Isaya 40:3. (Luka 3:1-6) Huku akiongozwa kwa kupuliziwa, Yohana aliyatumia maneno ya Isaya kujihusu mwenyewe. (Yohana 1:19-23) Kuanzia mwaka wa 29 W.K., Yohana alianza kuitayarisha njia kwa ajili ya Yesu Kristo.a Tangazo la mapema la Yohana liliwaamsha watu ili nao wapate kumtazamia Mesiya aliyeahidiwa, wamsikilize na kumfuata. (Luka 1:13-17, 76) Kupitia Yesu, Yehova angewaongoza wenye kutubu waingie katika uhuru ambao Ufalme wa Mungu pekee ndio uwezao kuuandaa—uhuru wa kutokuwepo kwa dhambi na kifo. (Yohana 1:29; 8:32)

  • ‘Wafarijini Watu Wangu’
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • a Isaya atabiri kutengenezwa kwa njia mbele za Yehova. (Isaya 40:3) Hata hivyo, Gospeli zahusisha unabii huo na yale ambayo Yohana Mbatizaji alifanya kumtayarishia Yesu Kristo njia. Waandikaji waliopuliziwa wa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo walifanya uhusiano huo kwa sababu Yesu alimwakilisha Baba yake naye alikuja katika jina la Baba yake.—Yohana 5:43; 8:29.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki