-
“Mtu Mwingine Hajapata Kamwe Kusema Kama Huyu”‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
-
-
Sura ya 11
“Mtu Mwingine Hajapata Kamwe Kusema Kama Huyu”
1, 2. (a) Kwa nini maofisa waliotumwa kumkamata Yesu walirudi mikono mitupu? (b) Ni nini kilichomfanya Yesu kuwa mwalimu wa pekee?
MAFARISAYO wamewaka hasira. Yesu yumo hekaluni akifundisha kumhusu Baba yake. Wanaomsikiliza wamegawanyika; wengi wanamwamini Yesu, lakini wengine wanataka akamatwe. Wakiwa wameshindwa kuzuia hasira yao, viongozi wa dini wanawatuma maofisa wakamkamate Yesu. Hata hivyo, maofisa hao wanarudi mikono mitupu. Wakuu wa makuhani na Mafarisayo wanauliza hivi kwa hasira: “Kwa nini hamkumleta?” Maofisa hao wanajibu: “Mtu mwingine hajapata kamwe kusema kama huyu.” Walivutiwa sana na mafundisho ya Yesu hivi kwamba hawakuona sababu ya kumkamata.a—Yohana 7:45, 46.
-
-
“Mtu Mwingine Hajapata Kamwe Kusema Kama Huyu”‘Njoo Uwe Mfuasi Wangu’
-
-
a Huenda maofisa hao walikuwa watumishi wa Sanhedrini waliokuwa chini ya mamlaka ya wakuu wa makuhani.
-