-
“Neno la Yehova Likaendelea Kukua”Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
6. Ni fungu gani la maneno linalohusiana na ukuzi ambalo hupatikana mara tatu katika kitabu cha Matendo, nalo hurejezea nini?
6 Njia moja ya kuchunguza utimizo wa Matendo 1:8 ni kufikiria usemi “neno la Yehova likaendelea kukua.” Fungu hili la maneno limetumiwa mara tatu tu katika Biblia, kwa kubadilishwa-badilishwa kidogo, kwenye kitabu cha Matendo peke yake. (Matendo 6:7; 12:24; 19:20) “Neno la Yehova,” au “neno la Mungu,” katika maandiko hayo larejezea habari njema—ujumbe wa kusisimua wa kweli ya Mungu, ujumbe wenye nguvu sana ambao ulibadili maisha ya wale walioukubali.—Waebrania 4:12.
-
-
“Neno la Yehova Likaendelea Kukua”Mnara wa Mlinzi—2001 | Aprili 1
-
-
Maeneo Yaongezeka
11. Ni ukuzi gani unaoelezwa kwenye Matendo 12:24, nao ulitukiaje?
11 Ukuzi wa neno la Mungu warejezewa mara ya pili kwenye Matendo 12:24: “Neno la Yehova likaendelea kukua na kusambaa.” Hapa fungu hilo la maneno lahusianishwa na ongezeko la maeneo yaliyohubiriwa. Licha ya upinzani wa serikali, kazi iliendelea kusitawi. Roho takatifu ilimwagwa kwanza Yerusalemu, na tokea hapo neno likasambaa haraka. Mnyanyaso huko Yerusalemu ulitawanya wanafunzi kwenda maeneo mbalimbali kotekote katika Yudea na Samaria. Matokeo yakawaje? “Wale waliokuwa wametawanywa walipita katika nchi wakitangaza habari njema ya lile neno.” (Matendo 8:1, 4) Filipo alielekezwa akamtolee ushahidi mwanamume mmoja ambaye, baada ya kubatizwa, alipeleka ujumbe hadi Ethiopia. (Matendo 8:26-28, 38, 39) Upesi kweli ilisitawi katika Lida, Uwanda wa Sharoni, na Yopa. (Matendo 9:35, 42) Baadaye, mtume Paulo alisafiri maelfu ya kilometa baharini na katika nchi kavu, akianzisha makutaniko kotekote katika nchi nyingi za Mediterania. Mtume Petro alienda Babiloni. (1 Petro 5:13) Miaka 30 baada ya roho takatifu kumwagwa siku ya Pentekoste, Paulo aliandika kwamba habari njema ilikuwa ‘imehubiriwa katika viumbe vyote chini ya mbingu,’ labda akirejezea ulimwengu uliojulikana wakati huo.—Wakolosai 1:23.
12. Wapinzani wa Ukristo walikiri nini kuhusu ukuzi wa neno la Mungu katika maeneo mbalimbali?
12 Hata wapinzani wa Ukristo walikiri kwamba neno la Mungu lilikuwa limesitawi kotekote katika Milki ya Roma. Kwa mfano, andiko la Matendo 17:6 lasema kwamba katika Thesalonike, kaskazini mwa Ugiriki, wapinzani walipaaza sauti kwa kusema: “Watu hawa ambao wamepindua dunia inayokaliwa wako hapa pia.” Isitoshe, mwanzoni mwa karne ya pili, Pliny Mchanga akiwa Bithinia, alimwandikia barua Maliki Mroma Trajan kuhusu Ukristo. Alilalamika hivi: “[Haupo] mijini tu, lakini umesambaza upotovu wake katika vijiji na nchi jirani.”
13. Upendo wa Mungu kwa wanadamu ulidhihirikaje kuhusiana na ukuzi katika maeneo mbalimbali?
13 Ukuzi katika maeneo mbalimbali ulikuwa udhihirisho wa upendo mwingi wa Yehova kwa wanadamu wanaoweza kukombolewa. Petro alipoona roho takatifu ikijidhihirisha kwa Kornelio mtu asiye Myahudi, alisema hivi: “Kwa hakika nahisi kwamba Mungu si mwenye ubaguzi, bali katika kila taifa mtu ambaye humhofu na kutenda uadilifu akubalika kwake.” (Matendo 10:34, 35) Naam, habari njema zilikuwa ujumbe kwa watu wote na zingali hivyo hata sasa, na ukuzi wa neno la Mungu katika maeneo mbalimbali uliwapa watu kila mahali fursa ya kuitikia upendo wa Mungu. Katika karne hii ya 21, neno la Mungu limesambaa karibu sehemu zote za dunia.
-