Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutetea Imani Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Desemba 1
    • 12. Ni hali zipi zilizowasukuma Paulo na Barnaba waseme kwa ujasiri huko Ikoniamu?

      12 Fikiria pia kielelezo cha Paulo na Barnaba. Andiko la Matendo 14:1, 2 lasema: “Katika Ikoniamu wakaingia pamoja katika sinagogi la Wayahudi na kusema kwa namna ambayo umati mkubwa wa Wayahudi na pia Wagiriki ukapata kuwa waamini. Lakini Wayahudi ambao hawakuamini wakazichochea na kuzivuta vibaya nafsi za watu wa mataifa dhidi ya akina ndugu.” Tafsiri ya Biblia Habari Njema yasema: “Lakini Wayahudi wengine waliokataa kuwa waumini walichochea na kutia chuki katika mioyo ya watu wa mataifa mengine ili wawapinge hao ndugu.” Kwa kutoridhika na kukataa kwao wenyewe ujumbe huo, Wayahudi wapinzani walianza kampeni ya mashtaka yasiyoweza kuthibitishwa, wakijaribu kuwafanya wasio Wayahudi wawabague Wakristo.a Lazima chuki yao kwa Ukristo iwe ilikuwa yenye kina kirefu kama nini! (Linganisha Matendo 10:28.)

  • Kutetea Imani Yetu
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Desemba 1
    • a Kichapo Matthew Henry’s Commentary on the Whole Bible chaeleza kwamba wapinzani Wayahudi “walijishughulisha na kuwaendea kimakusudi [wasio Wayahudi] waliowafahamu, na kuwaambia yale yote akili zao au nia zao mbaya zingeweza kutunga, ili kuwafanya wawe na maoni yenye kudharau na yasiyofaa kuhusu Ukristo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki