Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jifunze Jinsi ya Kukesha Kutoka kwa Mitume wa Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Januari 15
    • Matendo 16:6-10

  • Jifunze Jinsi ya Kukesha Kutoka kwa Mitume wa Yesu
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Januari 15
    • 6, 7. (a) Kulitukia nini Paulo na wasafiri wengine walipokaribia Bithinia? (b) Ni uamuzi gani ambao wanafunzi walichukua, na matokeo yakawaje?

      6 Wasafiri hao wenye bidii walielekea wapi? Mstari wa 7 unaeleza hivi: “Tena, walipofika Misia wakafanya jitihada za kuingia Bithinia, lakini roho ya Yesu haikuwaruhusu.” Kwa kuwa hawakuruhusiwa kuhubiri katika Asia, Paulo na wenzake walielekea upande wa kaskazini, wakikusudia kuhubiri katika majiji ya Bithinia. Hata hivyo, walipokaribia Bithinia, kwa mara nyingine tena Yesu alitumia roho takatifu ili kuwazuia. Kufikia hapo ni lazima wanaume hao walianza kuchanganyikiwa. Walijua ni ujumbe gani wangehubiri na jinsi ya kuuhubiri, lakini hawakujua wangehubiri wapi. Tunaweza kusema hilo kwa njia hii: Walikuwa wamebisha mlango unaoelekea Asia, lakini mlango huo haukufunguliwa. Walibisha mlango unaoelekea Bithinia, kwa mara nyingine tena mlango huo haukufunguliwa. Je, waliacha kubisha mlango? Hapana, wahubiri hao wenye bidii hawakuacha!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki