-
Lidia—Mwabudu wa Mungu Mkaribishaji-WageniMnara wa Mlinzi—1996 | Septemba 15
-
-
a Miongoni mwa majiji ya maana sana ya Makedonia, Filipi lilikuwa koloni ya kijeshi iliyostawi kwa kadiri fulani yenye kuongozwa na jus italicum (Sheria ya Kiitalia). Sheria hiyo iliwahakikishia Wafilipi haki zifananazo na zile zilizofurahiwa na wenyeji wa Roma.—Matendo 16:9, 12, 21.
-
-
Lidia—Mwabudu wa Mungu Mkaribishaji-WageniMnara wa Mlinzi—1996 | Septemba 15
-
-
Kuhubiri kwa Paulo Katika Filipi
Wapata mwaka wa 50 W.K., Paulo alifunga safari yake ya kwanza kwenda Ulaya na kuanza kuhubiri katika Filipi.a Alipofika jiji jipya, ilikuwa desturi ya Paulo kulizuru sinagogi na kuhubiria kwanza Wayahudi na wageuzwa-imani waliokusanyika huko. (Linganisha Matendo 13:4, 5, 13, 14; 14:1.) Hata hivyo, kulingana na vyanzo fulani vya habari, sheria ya Roma ilikataza Wayahudi wasifuate dini yao wakiwa ndani ya “mipaka mitakatifu” ya Filipi. Kwa hiyo, baada ya kupisha “siku kadha wa kadha” huko, siku ya Sabato wamishonari hao walipata mahali kando ya mto nje ya jiji ambapo ‘walidhani pana mahali pa kusali.’ (Matendo 16:12, 13) Huo yaonekana ulikuwa Mto Gangites. Huko wamishonari waliwapata wanawake tu, mmoja wao akiwa Lidia.
-