Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Lidia—Mwabudu wa Mungu Mkaribishaji-Wageni
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Septemba 15
    • “Mwenye Kuuza Rangi ya Zambarau”

      Lidia aliishi Filipi, jiji kubwa la Makedonia. Hata hivyo, alikuwa ametoka Thiatira, jiji la eneo la Lidia, katika Asia Ndogo magharibi. Kwa sababu hiyo wengine hudokeza kwamba “Lidia” lilikuwa lakabu alilopewa huko Filipi. Yaani, alikuwa “Mlidia,” sawa na vile yule mwanamke ambaye Yesu Kristo alimtolea ushahidi alivyoitwa “mwanamke Msamaria.” (Yohana 4:9) Lidia aliuza “zambarau” au bidhaa zilizotiwa rangi hiyo. (Matendo 16:12, 14) Kuwako kwa watengenezaji wa rangi katika Thiatira na katika Filipi kwathibitishwa na maandishi yaliyofukuliwa na waakiolojia. Yawezekana kwamba Lidia alikuwa amehama kwa sababu ya kazi yake, ama ili afanye kazi yake mwenyewe ama awe mwakilishi wa kampuni ya watengenezaji wa rangi Wathiatira.

      Rangi ya zambarau ilikuwa na vyanzo mbalimbali. Iliyokuwa ya bei ghali zaidi iliziduliwa kutoka kwa aina fulani za kombe za pwani. Kulingana na mshairi wa karne ya kwanza Mroma Martial, vazi la zambarau bora zaidi ya Tiro (kitovu kingine ambapo rangi hiyo ilitokezwa) lingeweza kugharimu kufikia sesterces 10,000, au dinari 2,500 kiwango kilicho sawa na mshahara wa mfanyakazi wa siku 2,500. Kwa wazi mavazi hayo yalikuwa vitu vya starehe ambavyo ni wachache tu wangeweza kununua. Kwa hiyo huenda ikawa kwamba Lidia alikuwa tajiri. Kwa vyovyote, aliweza kuwatolea ukaribishaji-wageni mtume Paulo na waandamani wake—Luka, Sila, Timotheo, na huenda wengine.

  • Lidia—Mwabudu wa Mungu Mkaribishaji-Wageni
    Mnara wa Mlinzi—1996 | Septemba 15
    • “Mwabudu wa Mungu”

      Lidia alikuwa “mwabudu wa Mungu” (NW), lakini huenda alikuwa mgeuzwa-imani wa Dini ya Kiyahudi aliyekuwa akitafuta kweli ya kidini. Ingawa alikuwa na kazi nzuri, Lidia hakuwa mwenye kufuatia vitu vya kimwili. Badala ya hivyo, alitenga wakati kwa ajili ya mambo ya kiroho. “Moyo wake ulifunguliwa na Bwana, ayatunze maneno yaliyonenwa na Paulo,” na Lidia akaikubali kweli. Kwa kweli, ‘alibatizwa yeye na nyumba yake.’—Matendo 16:14, 15.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki