Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupambana Sana kwa Ajili ya Habari Njema Huko Thesalonike
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
    • Kwa sababu hawakumpata Paulo, walianza kutafuta usaidizi kutoka kwa watawala wa kuu zaidi wa jiji. Hivyo “wakamkokota Yasoni na akina ndugu fulani na kuwapeleka kwa watawala wa jiji, wakipaaza sauti hivi: ‘Watu hawa ambao wameipindua dunia inayokaliwa wapo hapa pia.’”​—Matendo 17:5, 6.

      Kwa sababu lilikuwa ndilo jiji kuu la Makedonia, jiji la Thesalonike lilikuwa likijitawala kwa kadiri fulani. Sehemu ya mamlaka yake ilikuwa ni baraza la watu au baraza la wananchi ambalo lilishughulikia matatizo ya watu. “Watawala wa jiji,” au mapolitaki,b walikuwa maofisa wakuu walio na jukumu la kudumisha utaratibu na kutatua hali ambazo zingefanya Waroma waingilie kati na hivyo kufanya jiji lipoteze mapendeleo yake. Hivyo basi, watawala hao wa jiji wangekuwa na wasiwasi kusikia kwamba amani ya watu imeharibiwa na “watu hao waliosababisha fujo.”

  • Kupambana Sana kwa Ajili ya Habari Njema Huko Thesalonike
    Mnara wa Mlinzi—2012 | Juni 1
    • b Neno hilo halikupatikana katika maandishi ya Kigiriki. Hata hivyo, maandishi fulani yaliyokuwa na neno hilo yalivumbuliwa katika eneo la Thesalonike. Baadhi ya maandishi hayo yalikuwa na tarehe ya karne ya kwanza K.W.K., hivyo kuthibitisha masimulizi ya kitabu cha Matendo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki