-
“Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
-
-
Kuhani wa Cheo cha Juu Anania, wanaume wazee Wayahudi, na Tertulo walimshtaki Paulo rasmi mbele ya Feliksi kuwa ‘msumbufu na mwenye kufanya uchochezi wa uasi miongoni mwa Wayahudi.’ Walidai kwamba alikuwa kiongozi mkuu wa “farakano la Wanazareti”
-
-
“Mimi Nakata Rufani kwa Kaisari!”Mnara wa Mlinzi—2001 | Desemba 15
-
-
Wayahudi walisababu kwamba Paulo hakufundisha Dini ya Wayahudi, au dini inayokubalika kisheria (religio licita). Badala yake, mambo aliyofundisha yalipaswa kuonwa kuwa haramu, au hata ya uchochezi.
Pia walidai kwamba Paulo alikuwa ‘akifanya uchochezi wa uasi miongoni mwa Wayahudi wote katika dunia yote inayokaliwa.’ (Matendo 24:5) Muda mfupi kabla ya hapo, Maliki Klaudio aliwashutumu Wayahudi wa Alexandria kwa “kuchochea usumbufu ulimwenguni pote.” Visa hivyo vinafanana sana. ‘Myahudi angeshtakiwa kwa kosa hilo wakati wa utawala wa Klaudio au miaka ya mapema ya utawala wa Nero,’ asema mwanahistoria A. N. Sherwin-White. “Wayahudi walikuwa wakijaribu kumchochea gavana aone mahubiri ya Paulo kuwa sawa na kuvuruga amani na utengamano miongoni mwa Wayahudi wote katika Milki yake. Walijua kwamba magavana hawakutaka kuhukumu mtu kwa sababu za kidini pekee na hivyo wakajaribu kufanya mashtaka hayo yaonekane kuwa ya kisiasa.”
-