Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Iweni Wenye Kufanya Amani na Watu Wote”
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Oktoba 15
    • 13, 14. (a) Kwa nini hatushangai tunapopata upinzani? (b) Tunaweza kuwabariki jinsi gani wale wanaotutesa?

      13 Soma Waroma 12:14,

  • “Iweni Wenye Kufanya Amani na Watu Wote”
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Oktoba 15
    • 14 Badala ya kuwachukia wale wanaotutesa, tunajitahidi kuwafundisha, huku tukitambua kwamba huenda wengine wao wanatenda hivyo kwa kutojua. (2 Kor. 4:4) Tunajitahidi kutii shauri hili la Paulo: “Endeleeni kuwabariki wale wanaowatesa; muwe mkibariki wala msiwe mkilaani.” (Rom. 12:14) Njia moja ya kuwabariki wapinzani wetu ni kusali kwa ajili yao. Yesu alisema hivi katika Mahubiri yake ya Mlimani: “Endeleeni kuwapenda adui zenu, kuwafanyia mema wale wanaowachukia, kuwabariki wale wanaowalaani, kusali kwa ajili ya wale wanaowatusi.” (Luka 6:27, 28) Mtume Paulo alijua kutokana na maisha yake mwenyewe kwamba mtesaji anaweza kugeuka na kuwa mwanafunzi mwaminifu wa Kristo na mtumishi mwenye bidii wa Yehova. (Gal. 1:13-16, 23) Katika barua nyingine, Paulo alisema: “Tunapotukanwa, tunabariki; tunapoteswa, tunavumilia; tunapoharibiwa sifa, tunasihi.”—1 Kor. 4:12, 13.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki