Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Dhihirisha Mtazamo wa Akili wa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Septemba 1
    • Acheni kila mmoja wetu ampendeze jirani yake katika lililo jema kwa ajili ya kujengwa kwake.

  • Dhihirisha Mtazamo wa Akili wa Kristo
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Septemba 1
    • 6. Twaweza kuigaje jinsi Yesu alivyoitikia alipopingwa na kushutumiwa?

      6 Sifa nyingine nzuri ambayo Yesu alidhihirisha ni kwamba sikuzote alikuwa na fikira nzuri na matendo mazuri. Hakuruhusu kamwe mtazamo mbaya wa wengine uathiri mtazamo wake mzuri wa kumtumikia Mungu; nasi tusiuruhusu kamwe. Aliposhutumiwa na kunyanyaswa kwa maana alimwabudu Mungu kwa uaminifu, Yesu alivumilia kwa subira bila kulalamika. Alijua kuwa wale wanaojaribu kuwapendeza jirani zao “katika lililo jema kwa ajili ya kujengwa kwake” wanaweza kutarajia upinzani kutoka kwa ulimwengu usio na imani na usioelewa.

      7. Yesu alidhihirishaje subira, na kwa nini tufanye vivyo hivyo?

      7 Yesu alionyesha kwa njia nyingine mtazamo unaofaa. Hakukosa kamwe subira kwa Yehova bali alingojea kwa subira utimizo wa makusudi Yake. (Zaburi 110:1; Mathayo 24:36; Matendo 2:32-36; Waebrania 10:12, 13) Isitoshe, Yesu hakukosa kamwe subira kwa wafuasi wake. Aliwaambia hivi: “Mjifunze kutoka kwangu”; na kwa kuwa alikuwa “mwenye tabia-pole,” maagizo yake yalijenga na kuburudisha. Na kwa vile alikuwa wa “hali ya chini moyoni,” hakuwa kamwe mwenye majivuno au kiburi. (Mathayo 11:29) Paulo atutia moyo tuige sifa hizo za mtazamo wa Yesu asemapo hivi: “Tunzeni mtazamo huu wa akili ndani yenu uliokuwa pia ndani ya Kristo Yesu, ambaye, ijapokuwa alikuwa akiwako katika umbo la Mungu, hakufikiria upokonyaji, yaani, kwamba yeye awe sawa na Mungu. La, bali alijifanya mwenyewe kuwa mtupu na kuchukua umbo la mtumwa na kuja kuwa katika ufanani wa wanadamu.”—Wafilipi 2:5-7.

      8, 9. (a) Kwa nini ni lazima tujitahidi kusitawisha mtazamo usio na ubinafsi? (b) Mbona tusivunjike moyo tunaposhindwa kufuata kikamilifu kiolezo alichotuachia Yesu, na Paulo aliwekaje kielelezo kizuri kwa habari hiyo?

      8 Ni rahisi kusema kwamba twataka kuwatumikia wengine nasi twataka kutanguliza mahitaji yao kabla ya yetu. Lakini tunapouchunguza kwa unyofu mtazamo wetu wa akili, huenda tukatambua kwamba mioyo yetu haielekei kufanya hivyo kikamilifu. Kwa nini? Kwanza, ni kwa sababu tumerithi tabia ya ubinafsi kutoka kwa Adamu na Hawa; pili, ni kwa sababu twaishi katika ulimwengu unaoendeleza ubinafsi. (Waefeso 4:17, 18) Ili kukuza mtazamo usio na ubinafsi, mara nyingi tunahitaji kusitawisha njia ya kufikiri ambayo ni kinyume cha hali yetu ya asili isiyokamilika. Hilo huhitaji azimio na jitihada.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki