-
Nanga Yao Ni Tumaini, Nao Huchochewa na UpendoMnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
-
-
Tumaini Linalolinganishwa na Nanga
10, 11. Paulo alilinganisha tumaini letu na nini, na kwa nini ulinganisho huo ulifaa?
10 Paulo alionyesha kwamba Yehova alitoa ahadi ya baraka ambazo zingekuja kupitia Abrahamu. Kisha mtume huyo akaeleza hivi: “Mungu . . . aliingia kwa kiapo, ili, kupitia mambo mawili yasiyobadilika [neno lake na kiapo chake] ambayo katika hayo haiwezekani Mungu kusema uwongo, sisi ambao tumekimbia hadi kwenye kimbilio tupate kuwa na kitia-moyo chenye nguvu tukishikilia tumaini lililowekwa mbele yetu. Tumaini hili tunalo kama nanga ya nafsi, likiwa hakika na imara.” (Waebrania 6:17-19; Mwanzo 22:16-18) Tumaini lililowekwa mbele ya Wakristo watiwa-mafuta ni la kupata uhai usioweza kufa huko mbinguni. Leo, watumishi wa Yehova walio wengi wana tumaini zuri ajabu la kupata uhai udumuo milele katika dunia paradiso. (Luka 23:43) Pasipo tumaini hilo, mtu hawezi kuwa na imani.
11 Nanga ni kifaa cha usalama chenye nguvu, ambacho ni lazima kitumiwe ili kuzuia meli isijongeejongee wala kuchukuliwa na maji. Hakuna baharia yeyote awezaye kuondoka bandarini bila nanga. Kwa kuwa Paulo alivunjikiwa na meli mara kadhaa, mwenyewe alijionea kuwa mara nyingi maisha ya mabaharia yalitegemea nanga za meli zao. (Matendo 27:29, 39, 40; 2 Wakorintho 11:25) Meli za karne ya kwanza hazikuwa na mtambo wa injini wa kumsaidia nahodha aziendeshe atakavyo. Isipokuwa meli za kivita zilizoendeshwa kwa makasia, mwendo wa vyombo ulitegemea upepo hasa. Ikiwa meli ya nahodha ingekabili hatari ya kugonga miamba, uchaguzi pekee aliokuwa nao ni kutia nanga na kungojea dhoruba ikwishe, huku akitumaini kuwa nanga haingechomoka kwenye sakafu ya bahari. Kwa hiyo Paulo alilinganisha tumaini la Mkristo na “nanga ya nafsi, likiwa hakika na imara.” (Waebrania 6:19) Tushambuliwapo na dhoruba za upinzani au tupatapo majaribu mengine, tumaini letu zuri ajabu ni kama nanga inayotuweka imara tukiwa nafsi hai, ili meli yetu ya imani isichukuliwe hadi kwenye sehemu hatari, ya kina kifupi, yenye shaka au ya miamba hatari ya uasi-imani.—Waebrania 2:1; Yuda 8-13.
12. Twaweza kuepukaje kujiondoa kwa Yehova?
12 Paulo aliwaonya Wakristo Waebrania hivi: “Jihadharini, akina ndugu, kwa kuhofu kusije kamwe kukasitawi katika yeyote kati yenu moyo mwovu unaokosa imani kwa kujiondoa kwa Mungu aliye hai.” (Waebrania 3:12) Katika maandishi ya Kigiriki, neno “kujiondoa” lamaanisha kihalisi “kusonga kando,” yaani kuasi imani. Walakini twaweza kuepuka huko kuvunjikiwa meli kubaya. Imani na tumaini vitatusaidia kushikamana na Yehova hata kunapokuwa na dhoruba kali sana ya majaribu. (Kumbukumbu la Torati 4:4; 30:19, 20) Imani yetu haitakuwa kama meli inayopeperushwa huku na huku kwa pepo za mafundisho ya uasi-imani. (Waefeso 4:13, 14) Nasi tukiwa na tumaini likiwa kama nanga yetu, tutaweza kustahimili dhoruba za maisha tukiwa watumishi wa Yehova.
-
-
Nanga Yao Ni Tumaini, Nao Huchochewa na UpendoMnara wa Mlinzi—1999 | Julai 15
-
-
Kusonga Mbele Kuelekea Shabaha Yetu!
18. Ni nini kitakachotusaidia kuvumilia mitihani yoyote ya wakati ujao ya imani yetu?
18 Imani yetu na upendo wetu vyaweza kutahiniwa vikali kabla ya kufika mfumo mpya wa mambo. Hata hivyo, Yehova ametuandalia nanga iliyo “hakika na imara”—tumaini letu zuri ajabu. (Waebrania 6:19; Waroma 15:4, 13) Upinzani na majaribu mengine vitupigapo kwa kurudiarudia, twaweza kuvumilia ikiwa tumelindwa na nanga ya tumaini letu. Baada ya wimbi moja la dhoruba kutulia na kabla jingine halijaanza, na tuazimie kutia nguvu tumaini letu na kuimarisha imani yetu.
-