Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Usitenganishe Kile Ambacho Mungu Ameunganisha
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Mei 1
    • Mke Mkristo anapaswa kuonyesha “roho ya utulivu na ya upole,” wala hapaswi kupinga mamlaka ya mume wake kwa kiburi au kujiamulia mambo kivyake. (1 Petro 3:4)

  • Usitenganishe Kile Ambacho Mungu Ameunganisha
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Mei 1
    • 16. Wake Wakristo wanaweza kujifunza nini kutokana na Sara na Rebeka?

      16 Kuwa na roho ya utulivu na upole hakumaanishi kwamba mwanamke Mkristo hana maoni yake mwenyewe au kwamba mawazo yake hayafai. Wanawake wa zamani waliomwogopa Mungu kama vile Sara na Rebeka, walichukua hatua ya kueleza mahangaiko yao kuhusu mambo, na masimulizi ya Biblia yanaonyesha kwamba Yehova aliunga mkono hatua walizochukua. (Mwanzo 21:8-12; 27:46–28:4) Wake Wakristo pia wanaweza kueleza hisia zao. Hata hivyo, wanapaswa kufanya hivyo kwa ufikirio wala si kwa madharau. Inaelekea kwamba mazungumzo ya aina hiyo yatakuwa yenye kupendeza na yenye matokeo zaidi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki