-
Jihadharini na Walimu Wasio wa Kweli!Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
-
-
3. Ni jambo gani lililotukia wakati uliopita ambalo Petro asema litatukia tena?
3 Baada ya Petro kuwahimiza ndugu zake wakazie uangalifu unabii, yeye asema hivi: “Hata hivyo, kulikuja pia kuwa na manabii wasio wa kweli [katika Israeli la kale], kama pia kutakavyokuwa na walimu wasio wa kweli miongoni mwenu.” (2 Petro 1:14–2:1) Watu wa Mungu wa nyakati za kale walipokea unabii wa kweli, lakini pia walilazimika kushindana na mafundisho yenye kufisidi ya manabii wasio wa kweli. (Yeremia 6:13, 14; 28:1-3, 15) “Katika manabii wa Yerusalemu,” akaandika Yeremia, “nimeona neno linalochukiza sana; hufanya zinaa; huenenda katika maneno ya uongo.”—Yeremia 23:14.
4. Kwa nini walimu wasio wa kweli wanastahili uangamizo?
4 Akifafanua yale ambayo walimu wasio wa kweli wangefanya katika kutaniko la Kikristo, Petro asema hivi: “Hawahawa wataleta ndani kimya-kimya mafarakano yenye kuangamiza na watakana hata mmiliki [Yesu Kristo] aliyewanunua, wakijiletea wenyewe uangamizo wa kasi.” (2 Petro 2:1; Yuda 4) Tokeo la mwisho la ufarakano huo wa karne ya kwanza ni Jumuiya ya Wakristo kama tunavyoijua leo.
-
-
Jihadharini na Walimu Wasio wa Kweli!Mnara wa Mlinzi—1997 | Septemba 1
-
-
Kuanzisha Mafundisho Yasiyo ya Kweli
6. Ni nini huwachochea walimu wasio wa kweli, nao hujaribuje kupata wanachotaka?
6 Kwa hekima, twaona jinsi ambavyo walimu wasio wa kweli huanzisha kufikiri kwao kulikofisidiwa. Kwanza Petro asema kwamba wanafanya hilo kimya-kimya, au katika njia ya kujificha, ya hila.
-