-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mifanano ya nzige ilishabihi farasi walio tayari kwa ajili ya pigano; na juu ya vichwa vyao palikuwa na kilichoonekana kuwa mataji kama dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu,
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
14. Ni kwa nini elezo la Yohana kuhusu hao nzige lilikifaa kile kikundi cha Wakristo waliohuishwa katika 1919?
14 Hii hutoa vizuri kielezi cha kikundi kishikamanifu cha Wakristo waliohuishwa katika 1919. Kama farasi, walikuwa tayari kwa ajili ya pigano, wakiwa na hamu nyingi ya kupigania ukweli katika njia aliyoeleza mtume Paulo. (Waefeso 6:11-13; 2 Wakorintho 10:4) Juu ya vichwa vyao Yohana huona kinachoonekana kuwa mataji kama ya dhahabu. Haingefaa wao kuwa na taji halisi kwa sababu wao hawaanzi kutawala wakati wangali duniani. (1 Wakorintho 4:8; Ufunuo 20:4) Lakini katika 1919 wao tayari walikuwa na mwonekano wa kifalme. Wao walikuwa ndugu za Mfalme, na mataji yao ya kimbingu walikuwa wamewekewa akiba maadamu wao wangeendelea kuwa waaminifu mpaka mwisho.—2 Timotheo 4:8; 1 Petro 5:4.
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Pia wao wana nyuso kama za wanadamu, sura hii ikielekeza kwenye sifa ya upendo kwa kuwa mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu, ambaye ni upendo. (Mwanzo 1:26; 1 Yohana 4:16)
-