-
Yohana Aona Yesu AliyetukuzwaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
12. Ni nini maana ya ule “upanga mkali, mrefu na wenye makali mawili”?
12 “Na katika mkono wake wa kulia alikuwa na nyota saba na katika kinywa chake upanga mkali, mrefu na wenye makali mawili ulitokeza, na wajihi wake ulikuwa kama jua wakati linapong’aa katika nguvu zalo. Na mimi nilipoona yeye, mimi nilianguka kama mfu kwenye nyayo zake.” (Ufunuo 1:16, 17a, NW) Baadaye kidogo, Yesu mwenyewe anaeleza maana ya hizo nyota saba. Lakini ebu angalia kinachotokeza katika mdomo wake: “Upanga mkali, mrefu na wenye makali mawili.” Ni sura yenye kufaa kama nini! Kwa maana Yesu ndiye aliyewekwa rasmi atamke hukumu za mwisho za Yehova dhidi ya adui Zake. Matamko yenye kukata maneno kutoka kinywa chake hutokeza kufishwa kwa waovu wote.—Ufunuo 19:13, 15.
13. (a) Wajihi wa Yesu, mwangavu na wenye kuangaza hutukumbusha sisi nini? (b) Tunapata chapa gani yote kutokana na elezeo la Yohana juu ya Yesu?
13 Wajihi wa Yesu ulio mwangavu, wenye kuangaza hutukumbusha sisi kwamba uso wa Musa ulitokeza miale yenye kuangaza Yehova alipokuwa amezungumza naye juu ya Mlima Sinai. (Kutoka 34:29, 30) Kumbuka, pia, kwamba wakati Yesu alipogeuka sura mbele ya mitume wake watatu karibu miaka 2,000 iliyopita, “uso wake uliangaza kama jua, na mavazi yake ya nje yakawa maangavu kama nuru.” (Mathayo 17:2, NW) Sasa, katika mwakilisho wa kinjozi wa Yesu katika kipindi cha hii siku ya Bwana, hali kadhalika uso wake unarudisha ubora wenye kung’aa wa mmoja ambaye amekuwa katika kuwapo kwa Yehova. (2 Wakorintho 3:18) Kwa kweli, chapa yote inayopelekwa na njozi ya Yohana ni ile ya mng’ao wa utukufu. Kutoka nywele nyeupe kama theluji, macho yenye kutoa mwali wa moto, na wajihi wenye kung’aa mpaka chini kwenye nyayo zenye mwako, ni njozi yenye ubora unaopita wote ya Mmoja ambaye sasa hukaa “katika nuru isiyoweza kukaribiwa.” (1 Timotheo 6:16)
-
-
Kufungua Kufuli ya Siri TakatifuUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Zile Nyota na Vile Vinara vya Taa
5. Yesu anaelezaje “zile nyota saba” na “vile vinara vya taa saba”?
5 Yohana amemwona Yesu akiwa katikati ya vinara vya taa saba vya dhahabu akiwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia. (Ufunuo 1:12, 13, 16) Sasa Yesu anaeleza hilo: “Kwa habari ya siri takatifu ya zile nyota saba ambazo wewe uliona juu ya mkono wangu wa kulia, na ya vile vinara vya taa saba vya dhahabu: Zile nyota saba humaanisha malaika wa yale makundi saba, na vile vinara vya taa saba humaanisha makundi saba.”—Ufunuo 1:20, NW.
6. Ni kitu gani kinachowakilishwa na hizo nyota saba, na ni kwa sababu gani jumbe zilielekezwa hasa kwa hizo?
6 Zile “nyota” ni “malaika wa yale makundi saba.” Katika Ufunuo, nyakati nyingine nyota hufananisha malaika halisi, lakini haielekei kwamba Yesu angetumia mwandikaji wa kibinadamu awaandikie viumbe wa roho wasioonekana. Kwa hiyo zile “nyota” lazima ziwe wale waangalizi wa kibinadamu, au wazee, katika makundi, wakionwa kuwa wajumbe wa Yesu.b Hizo nyota zinapelekewa jumbe, kwa kuwa hizo zina daraka la kuangalia kundi la Yehova.—Matendo 20:28.
7. (a) Ni jambo gani linaloonyesha kwamba Yesu anaposema kwa malaika mmoja hilo halimaanishi kwamba kila kundi lina mzee mmoja tu? (b) Ni nani, kwa kweli, wanaowakilishwa na zile nyota saba katika mkono wa kulia wa Yesu?
7 Kwa kuwa Yesu anasema kwa “malaika” mmoja tu katika kila kundi, je! hilo linamaanisha kwamba kila kundi lina mzee mmoja tu? La. Mapema kama siku ya Paulo, kundi la Efeso lilikuwa na wazee kadhaa, si mmoja tu. (Ufunuo 2:1; Matendo 20:17) Kwa hiyo katika siku ya Yohana, wakati nyota saba zilipopelekewa jumbe zikasomwe kwenye yale makundi (kutia na kundi la Efeso), nyota hizo lazima ziwe zilisimama badala ya wale wote waliotumikia katika mabaraza ya wazee ndani ya kundi lililopakwa mafuta la Yehova. Hali kadhalika, waangalizi leo husomea makundi barua zinazopokewa kutoka Baraza Linaloongoza, ambalo washiriki walo ni waangalizi wapakwa-mafuta wanaotumikia chini ya ukichwa wa Yesu. Mabaraza ya wazee ya kienyeji yapaswa yahakikishe kwamba shauri la Yesu linafuatwa na makundi yao. Bila shaka, shauri linatolewa kwa manufaa ya wale wote wanaoshirikiana na kundi, na si wazee tu.—Ona Ufunuo 2:11a.
8. Ni jambo gani linaloonyeshwa na wazee kuwa katika mkono wa kulia wa Yesu?
8 Kwa kuwa Yesu ndiye Kichwa cha kundi, wazee wanasemwa kwa kufaa kuwa wamo katika mkono wake wa kulia, yaani, chini ya udhibiti na mwelekezo wake. (Wakolosai 1:18) Yeye ndiye Mchungaji Mkuu, nao ni wachungaji walio chini yake.—1 Petro 5:2-4.
-