Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kwa kufaa, hao mashahidi wawili wanaonwa sasa wakifanya ishara zinazokumbusha zile za Musa na Eliya. Mathalani, Yohana anasema hivi kwa habari yao: “Na ikiwa yeyote anataka kudhuru wao, moto hutoka katika vinywa vyao na kuwala adui zao; na ikiwa yeyote angepaswa kutaka kudhuru wao, kwa jinsi hii yeye lazima auawe. Hawa wana mamlaka kufunga mbingu ili kwamba mvua isianguke wakati wa kutoa kwao unabii.”—Ufunuo 11:5, 6a, NW.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 17. (a) Ni matukio gani katika siku za Eliya yaliyohusu ukame na moto? (b) Moto ulitokaje katika vinywa vya mashahidi wawili, na ni ukame gani uliohusika?

      17 Vipi Eliya? Katika siku za wafalme wa Israeli, nabii huyu alipiga mbiu ya ukame kuwa wonyesho wa ghadhabu ya Yehova juu ya Waisraeli waabudu-Baali. Uliendelea kwa miaka mitatu na nusu. (1 Wafalme 17:1; 18:41-45; Luka 4:25; Yakobo 5:17) Baadaye, wakati Mfalme Ahazi alipotuma askari-jeshi wamlazimishe Eliya aje ndani ya kuwapo kwake kwa kifalme, nabii huyo aliita moto kutoka mbinguni uteketeze askari-jeshi hao. Ni wakati tu kamanda wa kivita alipoonyesha heshima inayofaa cheo chake akiwa nabii ndipo Eliya alikubali kuandamana naye kwenda kwa mfalme. (2 Wafalme 1:5-16) Hali kadhalika, kati ya 1914 na 1918, baki la wapakwa-mafuta lilivuta uangalifu kwa ujasiri kwenye hali ya ukame wa kiroho katika Jumuiya ya Wakristo na likaonya juu ya hukumu yenye moto kwenye “ile siku kubwa na yenye kuvuvia hofu ya Yehova inayokuja.”—Malaki 4:1, 5; Amosi 8:11, NW.

      18. (a) Ni mamlaka gani waliyopewa mashahidi wawili, na ni jinsi gani ni kama ile aliyopewa Musa? (b) Mashahidi wawili walifichuaje Jumuiya ya Wakristo?

      18 Yohana anazidi kusema hivi juu ya wale mashahidi wawili: “Na wao wana mamlaka juu ya maji kuyageuza kuwa damu na kupiga dunia kwa kila aina ya tauni mara nyingi kadiri watakavyo.” (Ufunuo 11:6b, NW) Ili kumsadikisha Farao aruhusu Israeli waende wakiwa huru, Yehova alitumia Musa apige Misri yenye uonevu kwa tauni kutia na kugeuza maji kuwa damu. Karne nyingi baadaye, Wafilisti adui za Israeli walikumbuka vizuri matendo ya Yehova dhidi ya Misri, hiyo ikiwafanya walie: “Ni nani ataokoa sisi kutoka mkono wa Mungu huyu mwenye fahari ya kifalme? Huyu ndiye yule Mungu ambaye alikuwa mpigaji wa Misri kwa kila aina ya uchinjaji [“mapigo,” Union Version] katika nyika.” (1 Samueli 4:8 NW; Zaburi 105:29) Musa alifananisha Yesu, ambaye alikuwa na mamlaka kutamka hukumu za Mungu juu ya viongozi wa kidini wa siku yake. (Mathayo 23:13; 28:18; Matendo 3:22) Na wakati wa vita ya kwanza ya ulimwengu ndugu za Kristo, wale mashahidi wawili, walifichua ile hali ya “maji” yenye kuleta kifo ambayo Jumuiya ya Wakristo ilikuwa ikiwapa makundi yayo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki