-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na wale wanaokaa juu ya dunia hushangilia juu yao na kujifurahisha wenyewe, na wao watapelekeana zawadi, kwa sababu manabii wawili hawa walitesa wale wanaokaa juu ya dunia.”—Ufunuo 11:7-10, NW.
-
-
Kuhuisha Mashahidi WawiliUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Picha katika ukurasa wa 168]
Kushangilia kwa Ufunuo 11:10
Katika kitabu chake Preachers Present Arms, kilichotangazwa katika 1933, Ray H. Abrams anarejezea upinzani mkali wa viongozi wa kidini kuelekea kitabu cha Wanafunzi wa Biblia The Finished Mystery. Yeye hupitia jitihada za viongozi wa kidini za kuondolea mbali Wanafunzi wa Biblia na “usadikishi [wao] wenye kusumbua sana.” Hiyo iliongoza kwenye kesi ya mahakamani iliyokuwa na tokeo la kuhukumia J. F. Rutherford na waandamani wenzake saba miaka mirefu gerezani. Dakt. Abrams anaongezea: “Uchanganuzi wa kesi yote hiyo unaongoza kwenye mkataa wa kwamba makanisa na viongozi wa kidini mwanzoni ndio walioanza mwendo wa kufutilia mbali Waruseli. Katika Kanada, katika Februari, 1918, makasisi walianza kampeni kamili dhidi yao na vichapo vyao, hasa The Finished Mystery. Kulingana na Tribune ya Winnipeg, . . . kukandamizwa kwa kitabu chao kuliitikadiwa kuwa kuliletwa moja kwa moja na ‘mawakilisho ya viongozi wa kidini.’”
Dakt. Abrams anaendelea: “Wakati habari za hukumu ya vifungo hivyo vya miaka ishirini zilipowafikia wahariri wa magazeti ya kidini, karibu kila kimoja cha vichapo hivyo, kikubwa na kidogo, kilishangilia tukio hilo. Mimi nimeshindwa kuona maneno yoyote ya kusikitikia katika lolote la majarida hayo ya dini zilizokubaliwa. ‘Hakuwezi kuwa na shaka,’ akakata maneno Upton Sinclair, kwamba ‘mnyanyaso . . . ulianza kwa sehemu kutokana na uhakika wa kwamba wao walikuwa wamejiletea chuki ya vikundi vya kidini “vilivyokubaliwa.”’ Kile ambacho jitihada za pamoja za makanisa zilikuwa zimeshindwa kufanya sasa inaonekana serikali ilikuwa imefaulu kuwatimizia.” Baada ya kunukuu maelezo yenye kuvunja heshima ya vichapo kadhaa vya kidini, mwandikaji huyo alirejezea badiliko la uamuzi katika Mahakama ya Rufani akaeleza: “Uamuzi huu ulipokewa na makanisa kwa ukimya.”
-