Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Lakini mataifa yakawa yenye kujaa hasira-kisasi, na hasira-kisasi yako ikaja, na wakati uliowekwa rasmi kwa ajili ya wafu kuhukumiwa, na wa kuwapa thawabu zao watumwa wako manabii na watakatifu na wale wanaohofu jina lako, wadogo na wakubwa, na kuleta kwenye angamizo wale wanaoangamiza dunia.” (Ufunuo 11:18, NW) Kuanzia 1914 na kuendelea mataifa ya ulimwengu yameonyeshana hasira-kisasi kwa ukali, na dhidi ya Ufalme wa Mungu, na hasa dhidi ya mashahidi wawili wa Yehova.—Ufunuo 11:13.

      9. Mataifa yamekuwa yakiangamizaje dunia, naye Mungu ameazimu kufanya nini juu ya hilo?

      9 Katika muda wote wa historia mataifa yamekuwa yakiangamiza dunia kwa vita vyao visivyokoma na kwa usimamizi mbaya. Hata hivyo, tangu 1914 angamizo hili limechapua mwendo kwa kiwango chenye kuhofisha. Pupa na ufisadi vimetokeza kuenea kwa majangwa na kupotezwa sana kwa bara lenye kuzaa. Mvua ya asidi na mawingu ya redioaktivu vimeharibu maeneo makubwa. Vyanzo vya chakula vimechafuliwa. Hewa tunayopumua na maji tunayokunywa yametiwa uchafu. Takataka za viwandani hutisha kumaliza uhai katika bara na bahari. Na wakati fulani, mataifa yenye nguvu zaidi yalitisha kuleta angamizo kamili kwa njia ya kufutilia mbali kabisa aina yote ya kibinadamu kwa vita ya nyukilia. Kwa furaha, Yehova ‘ataleta kwenye angamizo wale wanaoangamiza dunia’; yeye atatekeleza hukumu juu ya binadamu wale wenye kiburi, wenye kukana kuwako kwa Mungu ambao ndio wenye daraka kwa hali yenye kusikitisha ya dunia. (Kumbukumbu 32:5, 6; Zaburi 14:1-3) Kwa hiyo, Yehova anapangia ole wa tatu, ili kuleta watenda-kosa hawa kwenye kutozwa hesabu.—Ufunuo 11:14.

      Ole kwa Wenye Kuangamiza!

      10. (a) Ole wa tatu ni nini? (b) Ni kwa njia gani ole wa tatu huleta zaidi ya mateso tu?

      10 Basi, huu ndio ole wa tatu. Waja upesi! Ni njia ya Yehova ya kuleta kwenye angamizo wale wanaochafua “kibago cha nyayo” zake, dunia hii yenye kupendeza ambayo juu yayo sisi tunaishi. (Isaya 66:1, NW) Unaanzishwa mwendo na Ufalme wa Kimesiya—ile siri takatifu ya Mungu. Maadui wa Mungu, hasa viongozi wa Jumuiya ya Wakristo, wameteswa na zile ole mbili za kwanza—zinazotokana hasa na tauni ya nzige na majeshi ya wapanda-farasi lakini ole wa tatu, ambao unaletwa na Ufalme wa Yehova wenyewe, unaleta zaidi ya mateso tu. (Ufunuo 9:3-19) Unaandaa pigo la kifo katika kuondolea mbali jamii ya kibinadamu yenye kuangamiza pamoja na watawala wayo. Huu utakuja ukiwa upeo wa kuhukumu kwa Yehova penye Har–Magedoni. Ni kama Danieli alivyotoa unabii: “Na katika siku za wafalme hao [watawala ambao wanaangamiza dunia] Mungu wa mbingu atasimamisha ufalme ambao hautaletwa kamwe kwenye angamizo. Na ufalme wenyewe hautapitishwa kwa watu wengine wowote. Utaponda-ponda na kuweka mwisho kwenye falme zote hizi, na huo wenyewe utasimama hadi nyakati zisizo dhahiri.” Kama mlima mkubwa, Ufalme wa Mungu utatawala juu ya dunia iliyofanywa kuwa tukufu, ukitetea enzi kuu ya Yehova na ukileta shangwe ya milele kwa aina ya binadamu.—Danieli 2:35, 44, NW; Isaya 11:9; 60:13.

      11. (a) Unabii unaeleza habari ya mfululizo unaoendelea wa matukio gani yenye furaha? (b) Ni fadhili zisizostahiliwa gani zinazofikiwa, jinsi gani, zinafikiwa na nani?

      11 Ole wa tatu unaandamana na mfululizo wa matukio ya furaha ambayo yatasonga mbele kwa mwendeleo kupitia siku ya Bwana. Ni wakati ‘wa wafu kuhukumiwa, na wa Mungu kuwapa thawabu yao watumwa wake manabii na watakatifu na wale wanahofu jina lake.’ Hiyo inamaanisha ufufuo kutoka kwa wafu! Kwa watakatifu wapakwa-mafuta ambao walikuwa wamekwisha kulala katika kifo, hilo linatukia mapema katika siku ya Bwana. (1 Wathesalonike 4:15-17) Wakati uwadiapo watakatifu wanaobaki wanajiunga na hawa kwa ufufuo wa mara hiyo. Wengine vilevile wanathawabishwa, kutia na watumwa wa Mungu manabii wa nyakati za kale na wengine wote wa aina ya binadamu ambao wanakuja kuhofu jina la Yehova, wawe ni wa umati mkubwa ambao unaokoka dhiki kubwa au wa “wafu, wakubwa na wadogo,” ambao wanainuliwa kwenye uhai wakati wa Utawala wa Mileani wa Kristo. Kwa kuwa Mfalme wa Kimesiya wa Mungu ana funguo za kifo na za Hadesi, utawala wa Ufalme wake unamfungulia njia awape uhai wa milele wote wanaojitahidi kufikia uandalizi huo wenye thamani kubwa. (Ufunuo 1:18; 7:9, 14; 20:12, 13, NW; Warumi 6:22; Yohana 5:28, 29) Uwe ni uhai usioweza kufa katika mbingu au uhai wa milele duniani, zawadi hii ya uhai ni fadhili zisizostahiliwa kutoka kwa Yehova, ambazo kwa ajili yazo kila mpokeaji aweza kuwa mwenye kushukuru milele!—Waebrania 2:9.

  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 175]

      Kuangamiza Dunia

      “Kila nukta tatu kisehemu cha msitu asili wenye kuleta mvua ukubwa wa kiwanja cha mpira hutoweka. . . . Upotevu wa msitu asilia unaharibu maelfu ya aina za mimea na za wanyama.”—Illustrated Atlas of the World (Rand McNally).

      “Katika karne mbili za ukazi, [Maziwa Makubwa] yamekuwa pia dimbwi la takataka la ulimwengu lililo kubwa zaidi ya yote.”—The Globe and Mail (Kanada).

      “Katika Aprili 1986 mlipuko na moto kwenye kiwanda cha nguvu za nyukilia katika Chernobyl, Urusi, “ulikuwa ndio tukio la nyukilia lenye maana zaidi sana . . . tangu kubomiwa kwa Hiroshima na Nagasaki,” likitokeza “mnururisho mwingi wa muda mrefu katika hewa, udongo-juu na maji ya ulimwengu kama majaribio yote ya nyukilia na mabomu yaliyopata kulipuliwa.”—JAMA; The New York Times.

      Katika Minamata, Japani, kiwanda cha kemikali kilidondosha kemikali ya methilmekyuri ndani ya ghuba. Kula samaki na samakimagamba waliochafuliwa na mdondosho huo kulitokeza ugonjwa wa Minamata (UM) “ugonjwa wa neva wenye kusedeka. . . . Leo hii [1985], imehakikishwa rasmi kuwa watu 2578 kotekote Japani wana UM.”—International Journal of Epidemiology.

  • Siri Takatifu ya Mungu—Upeo Wayo Wenye Utukufu!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Picha katika ukurasa wa 176]

      Matamko Yenye Uzani kwenye Ufunuo 11:15-19 ni utangulizi wa njozi zinazofuata. Ufunuo 12 ni kirejeshi kinachokuza zaidi matangazo matukufu kwenye Ufunuo 11:15, 17. Sura ya 13 hutoa mandhari-nyuma ya 11:18, kwa kuwa hueleza habari ya asili na usitawi wa tengenezo la kisiasa la Shetani ambalo limeleta angamizo kwenye dunia. Sura za 14 na 15 hueleza kirefu hukumu zaidi za Ufalme zinazofunganishwa na kuvumishwa kwa tarumbeta ya saba na ole wa tatu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki