Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na yeye akazaa mwana, wa kiume, ambaye anapaswa kuchunga mataifa yote kwa ufito wa chuma. Na mtoto wake akadakwa mbali hadi kwa Mungu na kwenye kiti cha ufalme chake.

  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 12:5,

  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Mtoto ni “mwana, wa kiume.” Ni kwa nini Yohana anatumia usemi huu wa maradufu? Yeye anafanya hivyo kuonyesha kufaa kwa mtoto, uwezo wake wa kutawala mataifa kwa uweza wa kutosha. Unakazia pia jinsi uzawa huu ulivyo pindi ya tukio lenye maana sana, la shangwe! Una daraka la maana sana katika kuleta siri takatifu ya Mungu kwenye tamati. Kwani, mtoto huyu wa kiume hata ‘atachunga mataifa yote kwa ufito wa chuma’!

      12. (a) Katika Zaburi, Yehova aliahidi nini kiunabii kwa habari za Yesu? (b) Ni nini kinachofananishwa na huyo mwanamke kuzaa mwana “ambaye anapaswa kuchunga mataifa yote kwa ufito wa chuma”?

      12 Sasa, je! usemi huo unasikika kuwa wenye kuzoeleka? Ndiyo, Yehova aliahidi kiunabii kwa mintarafu ya Yesu: “Wewe utavunja wao kwa fimbo ya kifalme ya chuma, kana kwamba ni chombo cha mfinyanzi wewe utaponda wao vipande vipande.” (Zaburi 2:9, NW) Pia unabii ulitolewa kwa habari yake hivi: “Ufito wa imara yako Yehova atapeleka kutoka Sayuni, akisema: ‘Enda ukishinda katikati ya maadui wako.’” (Zaburi 110:2, NW) Kwa hiyo, uzawa ulioonwa na Yohana unahusu sana Yesu Kristo. La, si kuzaliwa kwa Yesu na bikira huko nyuma kabla ya karne ya kwanza ya Wakati wa Kawaida wetu; wala haungeweza kuwa ukirejezea kuinuliwa kwa Yesu tena kwenye uhai wa roho katika 33 W.K. Zaidi ya hilo, si uhamaji. Badala ya hivyo, ni uzawa wa Ufalme wa Mungu katika 1914 ukiwa uhalisi, Yesu akiwa—sasa katika mbingu kwa karibu karne 20—ameketishwa katika kiti cha ufalme akiwa Mfalme.—Ufunuo 12:10.

      13. Ni nini kinachofananishwa na huyo mtoto wa kiume ‘kudakwa mbali hadi kwa Mungu na kwenye kiti cha ufalme chake’?

      13 Yehova hangeweza kamwe kuruhusu Shetani ameze mke Wake au mwana Wake aliyezaliwa hivi sasa! Wakati wa uzawa, mtoto huyo wa kiume ‘anadakwa mbali kwa Mungu na hadi kwenye kiti cha ufalme chake.’ Yeye anakuja hivyo chini ya himaya ya Yehova, ambaye ataangalia kikamili huu Ufalme uliozaliwa hivi sasa, chombo Chake cha kutakasia jina Lake takatifu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki