Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kwa minajili hii mwe na nderemo, nyinyi mbingu na nyinyi ambao hukaa ndani yazo!’”—Ufunuo 12:10-12a, NW.

  • Ufalme wa Mungu Wazaliwa!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 20. Wakristo waaminifu wamemshindaje Shetani?

      20 Wakristo wapakwa-mafuta, wanaohesabiwa kuwa waadilifu “kwa sababu ya damu ya Mwana-Kondoo,” wanaendelea kutoa ushuhuda kwa Mungu na kwa Yesu Kristo ijapokuwa minyanyaso. Kwa zaidi ya miaka 120, hii jamii ya Yohana imekuwa ikielekeza kwenye lile suala kubwa linalohusiana na kukoma kwa majira ya Mataifa katika 1914. (Luka 21:24) Na sasa umati mkubwa unatumikia kishikamanifu kando yao. Hakuna wowote wa hawa ‘wanahofu wale wanaoua mwili lakini hawawezi kuua nafsi,’ kama vile maono ya maisha halisi ya Mashahidi wa Yehova katika wakati wetu yameonyesha tena na tena. Kwa neno la kinywa na kwa mwenendo unaofaa wa Kikristo, wao wameshinda Shetani, wakithibitisha bila ugeugeu kwamba yeye ni mwongo. (Mathayo 10:28; Mithali 27:11; Ufunuo 7:9, NW) Wanapofufuliwa kwenda katika mbingu, ni lazima Wakristo wapakwa-mafuta wawe na furaha kama nini, kwa kuwa Shetani hayuko juu kule ili kushtaki ndugu zao! Kweli kweli, ni wakati wa wingi wote wa malaika, kuitikia kwa shangwe mwito: “Mwe na nderemo, nyinyi mbingu na nyinyi ambao hukaa ndani yazo!”

      Ole wa Ushindani!

      21. Shetani ameleteaje dunia na bahari ole?

      21 Akiudhika kwa sababu ya ole wa tatu, sasa Shetani ananuia kusumbua aina ya binadamu kwa namna yake mwenyewe ya ole. Ni: “Ole kwa ajili ya dunia na kwa ajili ya bahari, kwa sababu Ibilisi amekuja chini kwa nyinyi, akiwa na kasirani kubwa, akijua yeye ana kipindi kifupi cha wakati.” (Ufunuo 12:12b, NW) Kutupwa kwa Shetani nje ya mbingu bila shaka kunamaanisha ole kwa dunia halisi, ambayo inaangamizwa na binadamu wenye ubinafsi walio chini ya udhibiti wake. (Kumbukumbu 32:5) Hata zaidi hivyo, sera ya Shetani ‘tawala au angamiza’ huleta ole kwa dunia ya ufananisho, muundo wa jamii ya kibinadamu, pamoja na bahari ya ufananisho, lile tungamo lenye msukosuko la aina ya binadamu yenyewe. Wakati wa vita viwili vya ulimwengu, hasira-kisasi ya Shetani ilionyeshwa kwa hasira-kisasi ya mataifa yaliyotiishwa chini yake, na milipuko ya hasira kali ya roho waovu kama hiyo inaendelea hadi leo hii—ingawa si kwa muda mrefu zaidi! (Marko 13:7, 8)

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki