-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Sasa hayawani-mwitu ambaye mimi niliona alikuwa kama chui, lakini nyayo zake zilikuwa kama zile za dubu, na kinywa chake kilikuwa kama kinywa cha simba. Na drakoni akampa hayawani nguvu zake na kiti cha ufalme chake na mamlaka kubwa.”—Ufunuo 13:1b, 2, NW.
3. (a) Ni hayawani gani wakali sana alioona nabii Danieli katika njozi? (b) Hayawani wakubwa mno wa Danieli 7 waliwakilisha nini?
3 Huyu hayawani wa kiajabu ni nini? Biblia yenyewe hutoa jibu. Kabla ya anguko la Babuloni katika 539 K.W.K., Danieli nabii Myahudi aliona njozi zilizohusu hayawani wakali sana. Kwenye Danieli 7:2-8, NW yeye anaeleza habari za hayawani wanne wakitoka baharini, wa kwanza akishabihi simba, wa pili dubu, wa tatu chui, na “ona kule! hayawani wa nne, mwenye kuhofisha na mwenye kutisha na mwenye nguvu isivyo kawaida . . . na alikuwa na pembe kumi.” Huyu ni sawa kabisa na hayawani aliyeonwa na Yohana wapata mwaka 96 W.K. Pia hayawani huyo ana hulka za simba, dubu, na chui, na ana pembe kumi. Ni nini ulio utambulisho wa wale hayawani wakubwa mno walioonwa na Danieli? Yeye anatuarifu: “Hayawani hawa wakubwa mno . . . ni wafalme wanne ambao watasimama katika dunia.” (Danieli 7:17, NW) Ndiyo, hayawani hao wanawakilisha “wafalme,” au serikali kubwa za kisiasa za dunia.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8. Ni kwa nini haipasi kushtusha kwa vile Uingereza-Amerika serikali kubwa ya uwili, inafananishwa na hayawani?
8 Lakini je! haishtushi kutambulisha serikali za kisiasa na hayawani-mwitu? Ndivyo baadhi ya wapinzani walivyodai wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, hadhi ya Mashahidi wa Yehova, wakiwa tengenezo na wakiwa watu mmoja mmoja, ilipokuwa ikitiliwa shaka katika mahakama za sheria kotekote duniani. Lakini tua ufikirie! Je! mataifa yenyewe hayatumii hayawani au viumbe-mwitu kuwa ishara za kitaifa zao? Mathalani, kuna simba wa Uingereza, tai wa Amerika, na drakoni wa Uchina. Basi sababu gani yeyote apinge ikiwa Mtungaji wa kimungu wa Biblia Takatifu anatumia pia hayawani kufananisha serikali za ulimwengu?
9. (a) Ni kwa nini mmoja hapaswi kupinga Biblia inaposema kwamba Shetani humpa hayawani-mwitu mamlaka yake kubwa? (b) Shetani anaelezwaje katika Biblia, naye anatumiaje uvutano juu ya serikali?
9 Zaidi ya hilo, sababu gani yeyote apinge Biblia inaposema kwamba Shetani ndiye anayewapa hawa hayawani-mwitu mamlaka yao kubwa? Mungu ndiye Chimbuko la taarifa hiyo, na mbele zake ‘mataifa ni kama tone kutoka ndoo na kama filamu tu ya vumbi.’ Mataifa hayo yangefanya vizuri kutafuta kibali cha Mungu kuliko kuudhikia njia ambayo Neno lake hueleza habari zayo. (Isaya 40:15, 17; Zaburi 2:10-12, NW) Shetani si mtu wa hadithi ya uwongo mwenye mgawo wa kuzitesa nafsi zilizoondoka katika moto. Hakuna mahali kama hapo. Badala ya hivyo, Shetani anaelezwa habari zake katika Maandiko kuwa “malaika wa nuru”—stadi wa udanganyi anayetumia uvutano wenye nguvu katika mambo ya kisiasa kwa ujumla.—2 Wakorintho 11:3, 14, 15; Waefeso 6:11-18.
-
-
Kupambana na Hayawani Wawili Wakali SanaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Vilevile angalia, drakoni ndiye “akampa hayawani nguvu zake na kiti cha ufalme chake na mamlaka kubwa.” (Linga Luka 4:6.) Hayawani huyo ni ubuni wa Shetani miongoni mwa matungamo ya aina ya binadamu. Kwa kweli Shetani ndiye “mtawala wa ulimwengu huu.”—Yohana 12:31, NW.
-