Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Washa Upya Upendo wa Kwanza!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kwa Waefeso, yeye ana ujumbe huu: “Mimi najua matendo yako, na kazi ngumu yako na uvumilivu, na ya kwamba wewe huwezi kuhimili watu wabaya, na ya kwamba uliwaweka kwenye mtihani wale ambao husema wao ni mitume, lakini wao sio, nawe uliwapata kuwa waongo.

  • Washa Upya Upendo wa Kwanza!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 2:2,

  • Washa Upya Upendo wa Kwanza!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Miaka fulani kabla ya hapa, mtume Paulo alikuwa ameonya wale wazee wa Efeso juu ya “mbwa-mwitu waonezi,” wasumbuaji wa kundi waasi-imani, naye alikuwa amewaambia wazee hao ‘waendelee kuamka,’ wakifuata kielelezo chake mwenyewe cha kutochoka. (Matendo 20:29, 31, NW)

  • Washa Upya Upendo wa Kwanza!
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 3. (a) “Mitume bandia” wametafutaje kudanganya waaminifu katika siku zetu? (b) Petro alitoa onyo gani juu ya waasi-imani?

      3 Katika kipindi cha ile siku ya Bwana, pia, wametokea “mitume bandia” ambao “husema mambo yaliyopopotoka ili kuvuta mbali wale wanafunzi baada yao wenyewe.” (2 Wakorintho 11:13; Matendo 20:30; Ufunuo 1:10, NW) Wao wanaona wema katika zile dini zote za kimafarakano, wakidai kwamba Mungu hana tengenezo, na kukana kwamba Yesu hakupokea uwezo wa Ufalme katika 1914. Wao hutimiza ule unabii kwenye 2 Petro 3:3, 4, NW: “Katika siku za mwisho watakuja wadhihaki pamoja na dhihaka yao, wakiendelea kulingana na tamaa zao wenyewe na kusema: ‘Ku wapi huku kuwapo kwake kulikoahidiwa? Kwani, tangu ile siku mababu wetu walipolala usingizi katika kifo, mambo yote yaendelea sawasawa kama yalivyokuwa tangu mwanzo wa kuumba.’”

      4. (a) Kiburi na uasi wa wadhihaki unadhihirishwaje? (b) Wakristo leo wanaonyesha kwamba wao wako kama Waefeso kwa kuchukua tendo gani dhidi ya wapinzani waongo?

      4 Wadhihaki hawa wanaasi lile wazo la kufanya tangazo la peupe la imani yao. (Warumi 10:10) Wao wametumia uungaji-mkono wa viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo na msaada wa majarida ya habari na stesheni za TV ili kueneza ripoti za uwongo kuhusu washirika wao wa hapo zamani. Upesi wale waaminifu wanapata kuona kwamba usemi na mwenendo wa wadanganyaji hawa hauna mlio wa ukweli. Kama vile Waefeso, Wakristo leo ‘hawawezi kuhimili watu wabaya,’ kwa hiyo wanawatenga na ushirika watoke katika makundi yao.a

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki