Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na yeye hufanya ishara kubwa, hivi kwamba amepaswa hata kufanya moto uje chini duniani kutoka katika mbingu katika mwono wa aina ya binadamu.” (Ufunuo 13:11-13, NW)

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 27. (a) Ni mwelekeo gani wa hayawani-mwitu mwenye pembe mbili unaoonyeshwa na uhakika wa kwamba yeye anafanya moto ushuke chini kutoka mbinguni? (b) Watu wengi wanaonaje kifani cha ki-siku-hizi cha huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili?

      27 Huyu hayawani-mwitu mwenye pembe mbili hufanya ishara kubwa, hata kufanya moto ushuke kutoka katika mbingu. (Linga Mathayo 7:21-23.) Hii ishara ya pili hukumbusha sisi juu ya Eliya, nabii wa Mungu wa kale ambaye alijitia katika ushindani na manabii wa Baali. Yeye alipoitisha moto ushuke kutoka katika mbingu kwa kufaulu katika jina la Yehova, ulithibitisha kupita shaka lolote kwamba yeye alikuwa nabii wa kweli na kwamba wale manabii wa Baali walikuwa bandia. (1 Wafalme 18:21-40) Kama hao manabii wa Baali, huyo hayawani-mwitu mwenye pembe mbili huhisi kwamba yeye ana vitambulisho vya kuwa nabii. (Ufunuo 13:14, 15; 19:20) Kwani, yeye hudai kwamba amezima kani za uovu katika vita viwili vya ulimwengu, na alishinda ule unaoitwa eti ukomunisti unaokana kuwako kwa mungu! Kweli kweli, wengi, hukiona kifani cha ki-siku-hizi cha hayawani-mwitu mwenye pembe mbili kuwa mlinda uhuru na kibubujiko cha vitu vizuri vya kimwili.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki