Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Na huyo mwanamke alikuwa amepambwa zambarau na nyekundu-nyangavu na alikuwa amerembwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu na katika mkono wake alikuwa na kikombe cha dhahabu ambacho kilikuwa kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 17:4

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 24. Ni kwa sababu gani inafaa kwamba Babuloni Mkubwa amevalia “zambarau na rangi-nyekundu-nyangavu” na “amepambwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu”?

      24 Babuloni Mkubwa amevalia “zambarau na nyekundu-nyangavu,” rangi za jamaa ya kifalme, na “amerembwa kwa dhahabu na jiwe la thamani na lulu.” Inafaa kama nini! Fikiria tu yale majengo yote mazuri mno, sanamu-umbo na taswira azizi, aikoni zenye bei sana, na vikorokoro vingine vya kidini, pamoja na kiasi ambacho ni vigumu kuitikadi cha mali na pesa, kisichohesabika ambacho dini za ulimwengu huu zimerundika. Iwe ni katika Vatikani, katika milki ya uevanjeli wa TV ambao kitovu chayo ni United States, au katika misikiti na mahekalu yenye kuvutia ya Mashariki, Babuloni Mkubwa amerundika kama tungamo—na nyakati nyingine akapoteza—ukwasi mwingi mno.

      25. (a) Ni nini kinachofananishwa na “kikombe cha dhahabu ambacho kilijaa vitu vya kunyarafisha?” (b) Ni katika maana gani kahaba wa ufananisho amelewa?

      25 Tazama sasa alicho nacho kahaba huyu mkononi mwake. Haikosi Yohana alitweta kwa mshangao kukiona—kikombe cha dhahabu “kimejaa vitu vya kunyarafisha na vitu visivyo safi vya uasherati wake”! Hiki ndicho kikombe ambacho ndani yacho mna “divai ya kasirani ya uasherati wake” ambacho kwa hicho amefanya mataifa yote yalewe. (Ufunuo 14:8; 17:4) Kwa nje kinaonekana kuwa chenye utajiri, lakini yaliyomo ni yenye kunyarafisha, si safi. (Linga Mathayo 23:25, 26.) Ndani kina mazoea yote machafu na uwongo mwingi ambao huyo kahaba mkubwa ametumia kutongoza mataifa na kuwaleta chini ya uvutano wake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki