Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Hapa ndipo elimu iliyo na hekima inapofaa: Vichwa saba humaanisha milima saba, ambako mwanamke huketi juu ya kilele. Na wako wafalme saba: watano wameanguka, mmoja yupo, mwingine hajawasili bado, lakini yeye awasilipo lazima yeye abaki kitambo kifupi.” (Ufunuo 17:9, 10, NW)

  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 2. Ni nini maana ya vichwa saba vya hayawani-mwitu rangi-nyekundu-nyangavu, na inakuwaje kwamba “watano wameanguka, mmoja yupo”?

      2 Vichwa saba vya hayawani-mwitu mkali sana husimamia “milima” saba, au “wafalme” saba. Semi zote mbili hutumiwa Kimaandiko kurejezea mamlaka za kiserikali. (Yeremia 51:24, 25; Danieli 2:34, 35, 44, 45) Katika Biblia, serikali za ulimwengu sita hutajwa kuwa zikiathiri mambo ya watu wa Mungu: Misri, Ashuru, Babuloni, Umedi-Uajemi, Ugiriki, na Roma. Kati ya hizi, tano zilikuwa tayari zimekuja na zikaenda kufikia wakati Yohana alipopokea Ufunuo, lakini Roma ilikuwa ingali sana serikali ya ulimwengu. Hii inalingana vizuri na maneno haya, “watano wameanguka, mmoja yupo.” Lakini namna gani juu ya “mwingine” aliyekuwa akitazamiwa kuja?

  • Kufisha Babuloni Mkubwa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 6. Ni milki zipi mpya kabisa zilizotokea, na ni ipi iliyopata kuwa yenye kufanikiwa zaidi sana?

      6 Hata hivyo, kufikia karne ya 15, nchi fulani zilikuwa zikijenga milki mpya kabisa. Ingawa baadhi ya serikali hizi mpya za kibepari zilipatikana katika maeneo ambayo hapo kwanza yalikuwa makoloni ya Roma, milki zazo hazikuwa mwendelezo vivi hivi wa Milki ya Roma. Ureno, Hispania, Ufaransa, na Uholanzi zote zikawa makao ya milki zilizotapakaa sana. Lakini iliyofanikiwa zaidi sana ilikuwa Uingereza, ambayo ikaja kusimamia milki kubwa mno ambayo juu yayo ‘jua halikutua kamwe.’ Milki hii ilienea katika nyakati mbalimbali juu ya sehemu kubwa ya Amerika Kaskazini, Afrika, India, na Esia Kusini-mashariki, pamoja na maeneo ya Pasifiki Kusini.

      7. Serikali ya ulimwengu ya uwili ilikujaje kuwako, na Yohana alisema ni kwa muda gani ‘kichwa’ au serikali ya ulimwengu ya saba ingeendelea?

      7 Kufikia karne ya 19, baadhi ya makoloni katika Amerika Kaskazini yalikuwa yamekwisha kujitenga na Uingereza yakaunda United States ya Amerika yenye kujitawala. Kisiasa, hitilafu fulani ziliendelea kati ya taifa jipya na iliyokuwa nchi-mama yao. Hata hivyo, vita ya ulimwengu ya kwanza ilizilazimisha hizo nchi zote mbili kutambua masilahi yazo ya pamoja na zikatia nguvu uhusiano maalumu kati yazo. Hivyo, namna ya serikali ya ulimwengu ya uwili ikatokea, ikiwa inafanyizwa na United States ya Amerika, sasa ikiwa ndilo taifa la ulimwengu lenye ukwasi zaidi sana, na Uingereza, kao la milki ya ulimwengu iliyo kubwa zaidi sana. Basi, hiki, ndicho ‘kichwa’ cha saba, au serikali kubwa ya ulimwengu, ambayo inaendelea mpaka ndani ya wakati wa mwisho na katika maeneo ambamo Mashahidi wa ki-siku-hizi wa Yehova walijiimarisha kwanza. Kikilinganishwa na utawala mrefu wa kichwa cha sita, hiki cha saba ‘chabaki kitambo kifupi’ mpaka Ufalme wa Mungu uangamizapo mataifa yote.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki