Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Hatia ya Damu Yenye Kutisha

      14. Ni nini anayotoa malaika kabambe kuwa ndiyo sababu ya ukali wa hukumu ya Yehova, na Yesu alisema nini hali moja na hivyo wakati alipokuwa duniani?

      14 Kwa kumalizia, malaika kabambe amwambia Yohana sababu ya Yehova kumhukumu Babuloni Mkubwa kwa ukali hivyo. “Ndiyo,” asema malaika, “katika yeye ilipatikana damu ya manabii na ya watakatifu na ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” (Ufunuo 18:24, NW) Alipokuwa duniani, Yesu aliambia viongozi wa kidini kwamba wao walistahili kutozwa hesabu kwa ajili ya “damu yote yenye uadilifu iliyomwagwa juu ya dunia, kutoka damu ya Abeli mwadilifu” na kuendelea. Kulingana na hilo, kizazi hicho kombokombo kiliharibiwa katika 70 W.K. (Mathayo 23:35-38, NW) Leo, kizazi kingine cha wanadini kinabeba hatia ya damu kwa ajili ya kunyanyasa watumishi wa Mungu.

      15. Kanisa Katoliki katika Ujeremani ya Nazi lilikuwaje na hatia ya damu katika visa viwili?

      15 Katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany, Guenter Lewy anaandika: “Wakati Mashahidi wa Yehova walipokandamizwa katika Bavaria Aprili 13 [1933] Kanisa hata lilikubali mgawo liliopewa na Wizara ya Elimu na Dini wa kuripoti juu ya washiriki wa farakano hilo walioendelea kuzoea dini hiyo iliyokatazwa.” Hivyo Kanisa Katoliki linashiriki daraka la kupelekwa kwa maelfu ya Mashahidi kwenye kambi za mateso; mikono yalo imetiwa madoa ya damu ya uhai wa mamia ya Mashahidi ambao walinyongwa. Wakati Mashahidi vijana, kama Wilhelm Kusserow, walipoonyesha kwamba wangekufa kijasiri kwa kupigwa risasi na kikosi cha wapiga risasi, Hitla aliamua kwamba kikosi cha wapiga risasi hakikuwafaa wakataaji kidhamira; kwa hiyo Wolfgang ndugu ya Wilhelm, akiwa na umri wa miaka 20, alikufa kwa njia ya gilotini. Wakati ule ule, Kanisa Katoliki lilikuwa likiwatia moyo vijana Wakatoliki Wajeremani wafe katika jeshi la bara-baba lao. Hatia ya damu ya hilo kanisa yaonekana wazi!

      16, 17. (a) Ni hatia gani ya damu ambayo ni lazima Babuloni Mkubwa ashtakiwe, na Vatikani ilikuwaje na hatia ya damu kuhusu Wayahudi waliouawa katika michinjo-chinjo ya Kinazi? (b) Ni katika njia gani moja ambayo kwayo dini bandia ina lawama kwa ajili ya kuuawa kwa mamilioni ya watu katika mamia ya vita katika nyakati zetu?

      16 Hata hivyo, unabii unasema kwamba lazima Babuloni Mkubwa ashtakiwe kwa damu ya “wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” Hakika hilo limekuwa kweli katika nyakati za ki-siku-hizi. Mathalani, kwa kuwa hila ya Katoliki ndiyo iliyomsaidia Hitla apate mamlaka katika Ujeremani, Vatikani inashiriki hatia ya damu iliyo mbaya sana juu ya Wayahudi milioni sita waliokufa katika michinjo-chinjo ya Kinazi. Na zaidi, katika nyakati zetu, watu zaidi ya milioni mia moja wameuawa katika mamia ya vita. Je! dini bandia ina lawama kwa habari hii? Ndiyo, kwa njia mbili.

      17 Njia moja ni kwamba vita vingi vinahusiana na tofauti za kidini. Mathalani, jeuri katika India kati ya Waislamu na Wahindu katika 1946-48 ilichochewa na dini. Mamia ya maelfu ya maisha yalipotea. Pambano kati ya Iraki na Irani katika miaka ya 1980 lilihusiana na tofauti za kimafarakano, kukiwa na mamia ya maelfu waliouawa. Jeuri kati ya Wakatoliki na Waprotestanti katika Ailandi ya Kaskazini imetwaa maelfu ya maisha. Akichunguza uwanja huu, mleta habari za magazetini C. L. Sulzberger alisema hivi katika 1976: “Ni ukweli wenye kuhuzunisha kwamba pengine nusu au zaidi ya vita vinavyopiganwa sasa kotekote katika ulimwengu ama kwa wazi ni mapambano ya kidini ama yanahusu mabishano ya kidini.” Kweli kweli, imekuwa hivyo muda wote wa historia yenye msukosuko ya Babuloni Mkubwa.

      18. Ni ipi njia ya pili ambayo kwayo dini za ulimwengu zina hatia ya damu?

      18 Ni ipi ile njia nyingine? Kwa maoni ya Yehova, dini za ulimwengu zina hatia ya damu kwa sababu hizo hazikufundisha kwa kusadikisha wafuasi wazo ukweli wa matakwa ya Yehova kwa ajili ya watumishi wake. Hizo hazikufundisha watu kwa kusadikisha kwamba waabudu wa kweli lazima wamwige Yesu Kristo na kuonyesha wengine upendo bila kujali asili yao ya kitaifa. (Mika 4:3, 5; Yohana 13:34, 35; Matendo 10:34, 35; 1 Yohana 3:10-12) Kwa sababu dini ambazo zinajumlika kuwa Babuloni Mkubwa hazikufundisha vitu hivi, wafuasi wazo wamevutwa kuingizwa ndani ya kizingo cha vita vya kimataifa. Lo! jinsi hilo lilivyokuwa wazi katika vile vita viwili vya ulimwengu vya nusu ya kwanza ya karne ya 20, ambavyo vyote viwili vilianza katika Jumuiya ya Wakristo na vikatokeza kuchinjana kwa wanadini! Ikiwa wote wanaodai kuwa Wakristo wangalishikamana na kanuni za Biblia, vita hivyo havingaliweza kutukia kamwe.

      19. Ni hatia ya damu gani yenye kutisha sana anayobeba Babuloni Mkubwa?

      19 Yehova anaweka lawama la umwagaji-damu huu wote kwenye nyayo za Babuloni Mkubwa. Ikiwa viongozi wa kidini, hasa wale walio katika Jumuiya ya Wakristo, wangalifundisha watu wao ukweli wa Biblia, umwagaji-damu mkubwa sana hivyo haungalitukia. Kwa kweli, basi, kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, Babuloni Mkubwa—yule kahaba mkubwa na milki ya ulimwengu ya dini bandia—lazima amjibu Yehova si kwa ajili ya “damu ya manabii na ya watakatifu” tu ambao yeye amenyanyasa na akaua bali pia kwa ajili “ya wale wote ambao wamechinjwa juu ya dunia.” Kweli kweli Babuloni Mkubwa anabeba hatia ya damu yenye kutisha sana. Na apotelee mbali wakati uharibifu wake unapotukia!

  • Kuomboleza na Kushangilia Mwisho wa Babuloni
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku katika ukurasa wa 270]

      Gharama ya Kuridhiana

      Guenter Lewy anaandika katika kitabu chake The Catholic Church and Nazi Germany: “Kama Ukatoliki wa Ujeremani tangu mwanzo ungalishikamana na mwongozo wa kupinga kwa dhati utawala wa Nazi, historia ya ulimwengu ingaliweza kuchukua mwendo tofauti. Hata kama mng’ang’ano huu ungalikosa mwishowe kabisa kumshinda Hitla na kuzuia uhalifu wake mwingi, kwa oni hili ungaliinua sana hadhi ya kiadili ya Kanisa hilo. Gharama ya kibinadamu kwa ukinzani huu ingalikuwa kubwa bila kukanika, lakini dhabihu hizo zingalikuwa zimetolewa kwa ajili ya kusudi kubwa zaidi ya yote. Hitla akiwa haungwi mkono nyumbani, yamkini hangalithubutu kwenda vitani na kihalisi mamilioni ya maisha yangaliokolewa. . . . Wakati Wajeremani wapinga Unazi walipoteswa mpaka kifo katika kambi za mateso za Hitla, wakati weledi wa Polandi walipochinjwa, wakati mamia ya maelfu ya Warusi walipokufa kama tokeo la kutendwa kama Untermenschen [nusu-binadamu] wa Kislavi, na wakati binadamu 6,000,000 walipouawa kimakusudi kwa kuwa ‘si Waarya,’ maofisa wa Kanisa Katoliki katika Ujeremani walitegemeza utawala uliokuwa ukifanya uhalifu huu. Papa katika Roma, kichwa cha kiroho na mwalimu wa kiadili mkuu zaidi ya wote wa Kanisa Katoliki la Roma, alikaa kimya.”—Kurasa 320, 341.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki