Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mbingu Mpya na Dunia Mpya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na yeye akasema kwa mimi: ‘Yamekwisha tukia! Mimi ndiye Alfa na Omega, mwanzo na mwisho.’”—Ufunuo 21:5, 6a, NW.

  • Mbingu Mpya na Dunia Mpya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kwani, ahadi hizi za Yehova ni hakika sana hivi kwamba yeye hunena kama tayari zilitimia: “Yamekwisha tukia!” Je! Yehova siye “Alfa na Omega . . . , Mmoja ambaye yuko na ambaye alikuwako na ambaye anakuja, yule Mweza Yote”? (Ufunuo 1:8, NW) Kweli kweli ndiye! Yeye mwenyewe hujulisha wazi: “Mimi ndiye wa kwanza na mimi ndiye wa mwisho, na mbali na mimi hakuna Mungu.” (Isaya 44:6, NW) Akiwa hivyo, yeye anaweza kuvuvia unabii na kuutimiza katika kila jambo dogo-dogo. Jinsi inavyoimarisha imani!

  • Mbingu Mpya na Dunia Mpya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • “Maji” kwa Wenye Kiu

      10. Ni “maji” gani ambayo Yehova anatoa, nayo yanasimamia nini?

      10 Yehova mwenyewe ndiye anayejulisha wazi: “Yeyote anayeona kiu mimi nitampa kutoka kibubujiko cha maji ya uhai bure.” (Ufunuo 21:6b, NW) Ili kuzima kiu hicho, lazima mtu awe anaona uhitaji wake wa kiroho na awe na nia ya kukubali “maji” ambayo Yehova huandaa. (Isaya 55:1; Mathayo 5:3) “Maji” yapi? Yesu mwenyewe alijibu swali hilo alipokuwa akitoa ushahidi kwa mwanamke kando ya kisima katika Samaria. Yeye alimwambia: “Yeyote ambaye hunywa kutoka maji ambayo mimi nitampa yeye hataona kiu kamwe hata, lakini maji ambayo mimi nitampa yeye yatakuwa ndani ya yeye kibubujiko cha maji kikibubujika kupatia uhai wa milele.” Hicho “kibubujiko cha maji ya uhai” hutiririka kutoka kwa Mungu kupitia Kristo akiwa andalio lake kwa ajili ya kurudisha aina ya binadamu kwenye uhai mkamilifu. Kama mwanamke Msamaria, yatupasa sisi kuwa wenye hamu nyingi kama nini kunywa sana kutokana na kibubujiko hicho! Na kama mwanamke huyo, yatupasa kuwa tayari kama nini kuacha mapendezi ya kidunia na kupendelea kuwaambia wengine habari njema!—Yohana 4:14, 15, 28, 29, NW.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki