Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Na jiji lina miraba minne, na urefu walo ni mkubwa kama upana walo. Na yeye akapima jiji kwa mwanzi, farlong’i elfu kumi na mbili; urefu na upana walo na kimo vi sawa.

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ufunuo 21:15-

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 7. Ni jambo gani lenye kutokeza kuhusu vipimo vya jiji hilo?

      7 Hili ni jiji lenye kutokeza kama nini! Mchemraba kamilifu farlong’i 12,000 (kilometa zapata 2,220) katika mzingo, likizungukwa na ukuta wa kyubiti 144, au meta 64, za kimo. Hakuna jiji halisi lingeweza kuwa na vipimo kama hivyo. Lingefunika eneo lenye ukubwa wa takribani mara 14 ya Israeli ya ki-siku-hizi, na lingeenda juu kama mnara kwa takribani kilometa 560 kuingia ndani ya anga la juu zaidi! Ufunuo ulitolewa kwa ishara. Kwa hiyo, vipimo hivi vinatuambia nini juu ya Yerusalemu Jipya la kimbingu?

  • Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aa
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Tarakimu 12 inayoonekana katika vipimo vya jiji—vyenye farlong’i 12,000 za urefu, upana, na kimo zikiwa sawa—hutumiwa kitamathali katika mazingira ya kitengenezo katika unabii wa Biblia. Kwa sababu hiyo, Yerusalemu Jipya ni mpango wa kitengenezo uliobuniwa vizuri sana kwa ajili ya kutimiza kusudi la Mungu la milele. Yerusalemu Jipya, pamoja na Mfalme Yesu Kristo, ni tengenezo la Ufalme wa Yehova. Halafu kuna umbo la jiji: mchemraba mkamilifu. Katika hekalu la Solomoni, Patakatifu Zaidi Sana, ulimokuwa uwakilisho wa kimfano wa kuwapo kwa Yehova, mlikuwamo mchemraba mkamilifu. (1 Wafalme 6:19, 20) Basi, inafaa kama nini kwamba Yerusalemu Jipya, likimulikwa na utukufu wa Yehova mwenyewe, huonwa kuwa mchemraba mkamilifu, wa kadiri kubwa! Vipimo vyalo vyote ni vyenye kusawazika kikamilifu. Ni jiji lisilo na kasoro za ukawaida, au taksiri.—Ufunuo 21:22.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki