-
Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Na jiji hilo halina uhitaji wa jua wala mwezi kung’aa juu yalo, kwa maana utukufu wa Mungu ulilinururisha, na taa yalo ilikuwa ni Mwana-Kondoo.” (Ufunuo 21:22, 23, NW)
-
-
Jiji Lenye Uzuri wa Kung’aaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
14. (a) Ni kwa nini Yerusalemu Jipya halihitaji jua na mwezi kung’aa juu yalo? (b) Unabii wa Isaya ulitabiri nini kwa habari ya tengenezo la ulimwengu wote mzima la Yehova, na Yerusalemu Jipya lahusikaje katika hili?
14 Utukufu wa Yehova ulipopita karibu na Musa kwenye Mlima Sinai, ulifanya uso wa Musa kung’aa kwa uangavu mkubwa sana hivi kwamba yeye alilazimika kuufunika usionwe na Waisraeli wenzake. (Kutoka 34:4-7, 29, 30, 33) Basi, wewe unaweza kuwazia uangavu wa jiji ambalo hunururishwa daima na utukufu wa Yehova? Jiji kama hilo halingeweza kuwa na wakati wa usiku. Halingekuwa na uhitaji wa jua wala mwezi halisi. Lingekuwa likitoa nuru kwa umilele. (Linga 1 Timotheo 6:16.) Yerusalemu Jipya huoshwa na aina kama hiyo ya uangavu wenye kung’aa. Kweli kweli, bibi-arusi huyu pamoja na Bwana-arusi Mfalme wake wanakuwa ndio jiji kuu la tengenezo la Yehova la ulimwengu wote mzima—“mwanamke” wake, “Yerusalemu juu”—ambaye kwa habari zake Isaya aliandika hivi: “Kwako wewe jua halitathibitika tena kuwa nuru wakati wa mchana, na kwa uangavu mwezi wenyewe hautakupa wewe nuru tena. Na lazima Yehova awe kwako wewe nuru yenye kudumu kwa wakati usio dhahiri, na Mungu wako uzuri wako. Jua lako halitashuka tena, wala mwezi wako hautafifia; kwa maana Yehova mwenyewe atakuwa kwa ajili yako nuru yenye kudumu kwa wakati usio dhahiri, na siku za kuomboleza kwako zitakuwa zimekwisha kuja kwenye utimilifu.”—Isaya 60:1, 19, 20; Wagalatia 4:26, NW.
-