Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 18, 19. (a) Huenda usemi “jeshi la mahali palipo juu” warejezea nani, nao wakusanywaje “katika shimo”? (b) Huenda “jeshi la mahali palipo juu” litazingatiwaje “baada ya muda wa siku nyingi”? (c) Yehova awazingatiaje “wafalme wa dunia”?

      18 Unabii wa Isaya sasa watia ndani mambo mengi zaidi, ukitaja utekelezaji wa mwisho wa kusudi la Yehova: “Itakuwa katika siku hiyo, BWANA ataliadhibu jeshi la mahali palipo juu katika mahali palipo juu, na wafalme wa dunia katika dunia; nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza; na baada ya muda wa siku nyingi watajiliwa.

  • Yehova Ni Mfalme
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • 19 Huenda usemi “jeshi la mahali palipo juu” warejezea roho waovu walio “watawala wa ulimwengu wa giza hili, . . . majeshi ya roho waovu katika mahali pa kimbingu.” (Waefeso 6:12) Hao wameathiri sana serikali za ulimwengu. (Danieli 10:13, 20; 1 Yohana 5:19) Lengo lao ni kuwageuza watu kutoka kwa Yehova na ibada yake safi. Wao wafaulu kama nini kushawishi Israeli kufuata mazoea machafu ya mataifa yanayowazunguka na hivyo wastahili hukumu ya Mungu! Lakini hatimaye ni lazima Shetani na roho wake waovu watoe hesabu kwa Mungu ageuzapo uangalifu wake kwao na kwa watawala wa dunia, “wafalme wa dunia katika dunia,” ambao wamewashawishi wamwache Mungu na kuvunja sheria zake. (Ufunuo 16:13, 14) Akizungumza kwa mfano, Isaya asema kwamba watakusanywa na ‘kufungwa katika gereza.’ “Baada ya muda wa siku nyingi,” labda Shetani na roho wake waovu (lakini si “wafalme wa dunia katika dunia”) waachiliwapo kwa muda mfupi mwishoni mwa Utawala wa Miaka Elfu wa Yesu Kristo, Mungu atawapa adhabu ya mwisho inayowafaa.—Ufunuo 20:3, 7-10.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki