-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mimi nikasikia sauti kubwa katika mbingu ikisema: ‘Sasa kumetukia wokovu na nguvu na ufalme wa Mungu wetu na mamlaka ya Kristo wake, kwa sababu mshtaki wa ndugu zetu amevurumishwa chini, ambaye huwashtaki mchana na usiku mbele za Mungu wetu!
-
-
Ufalme wa Mungu Wazaliwa!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Kumwita Shetani “mshtaki wa ndugu zetu” kunaonyesha kwamba, hata ingawa mashtaka yake dhidi ya Ayubu yalithibitishwa kuwa bandia, yeye alifuliza moja kwa moja kutilia shaka ukamilifu wa watumishi wa kidunia wa Mungu. Kwa wazi, yeye alirudia kwa pindi nyingi lile shtaka la kwamba mtu atatoa vyote alivyo navyo kwa kubadilishana na nafsi yake.
-