Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Matendo
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 15
    • Sehemu ya kwanza ya kitabu cha Matendo inazungumzia hasa utendaji wa mtume Petro, na sehemu ya mwisho inahusu mtume Paulo. Luka anatumia maneno yanayoonyesha kwamba alikuwapo matukio fulani yalipotukia. Tukikazia fikira ujumbe wa kitabu cha Matendo tutathamini hata zaidi nguvu za Neno la Mungu lililoandikwa kwa roho yake takatifu. (Ebr. 4:12) Kufanya hivyo kutatuchochea pia kujidhabihu na kutajenga imani yetu katika tumaini la Ufalme.

      PETRO ANATUMIA “FUNGUO ZA UFALME”

      (Matendo 1:1–11:18)

      Baada ya kupokea roho takatifu, mitume wanatoa ushahidi kwa ujasiri. Petro anatumia ufunguo wa kwanza kati ya “funguo za ufalme wa mbinguni” ili kuwafungulia mlango wa ujuzi na kuwapa Wayahudi na watu waliogeuzwa imani “waliokubali neno lake” nafasi ya kuingia katika Ufalme. (Mt. 16:19; Mdo. 2:5, 41) Mateso yanaongezeka na kuwatawanya wanafunzi, lakini hilo linafanya kazi ya kuhubiri ipanuke.

      Mitume katika Yerusalemu wanaposikia kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wanawatuma Petro na Yohana huko. Petro anatumia ufunguo wa pili anapowapa Wasamaria nafasi ya kuingia katika Ufalme. (Mdo. 8:14-17) Sauli wa Tarso anafanya mabadiliko ya kustaajabisha sana labda mwaka mmoja hivi baada ya Yesu kufufuliwa. Katika mwaka wa 36 W.K., Petro anatumia ufunguo wa tatu, na zawadi ya bure ya roho takatifu inamwagwa juu ya watu wasiotahiriwa wa mataifa.—Mdo. 10:45.

  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Matendo
    Mnara wa Mlinzi—2008 | Mei 15
    • HUDUMA YENYE BIDII YA PAULO

      (Matendo 11:19–28:31)

      Katika mwaka wa 44 W.K., Agabo anakuja Antiokia, ambako Barnaba na Sauli wamekuwa wakifundisha “kwa mwaka mzima.” Agabo anatabiri “njaa kali,” ambayo inakuja miaka miwili baadaye. (Mdo. 11:26-28) Barnaba na Sauli wanarudi Antiokia “baada ya kutimiza kikamili ile huduma ya misaada katika Yerusalemu.” (Mdo. 12:25) Katika mwaka wa 47 W.K., miaka 12 hivi baada ya Sauli kuwa Mkristo, Barnaba na Sauli wanatumwa na roho takatifu kwa safari ya umishonari. (Mdo. 13:1-4) Katika mwaka wa 48 W.K., wanarudi Antiokia, “walikokuwa wamekabidhiwa kwenye fadhili zisizostahiliwa za Mungu.”—Mdo. 14:26.

      Baada ya miezi tisa kupita, Paulo (ambaye pia anaitwa Sauli) anamchagua Sila kuwa mwandamani wake na wanaenda kwenye safari yake ya pili ya umishonari. (Mdo. 15:40) Timotheo na Luka wanajiunga na Paulo njiani. Luka anabaki Filipi naye Paulo anaendelea na safari mpaka Athene kisha Korintho, ambako anakutana na Akila na Prisila na kukaa huko kwa mwaka mmoja na miezi sita. (Mdo. 18:11) Paulo anawaacha Timotheo na Sila huko Korintho, naye anawachukua Akila na Prisila na kusafiri kwenda Siria mwanzoni mwa mwaka wa 52 W.K. (Mdo. 18:18) Akila na Prisila walienda naye mpaka Efeso, wakabaki huko.

      Baada ya kukaa Antiokia ya Siria kwa muda fulani, Paulo anaanza safari yake ya tatu mwaka wa 52 W.K. (Mdo. 18:23) “Neno la Yehova [linazidi] kukua na kusitawi” huko Efeso. (Mdo. 19:20) Paulo anakaa huko kwa miaka mitatu hivi. (Mdo. 20:31) Pentekoste ya mwaka wa 56 W.K., inampata Paulo Yerusalemu. Baada ya kukamatwa, anatoa ushahidi bila kuogopa mbele ya wenye mamlaka. Huko Roma, mtume huyo anawekwa chini ya kifungo cha nyumbani kwa miaka miwili (karibu mwaka wa 59-61 W.K.), na akiwa huko anatafuta njia za kuhubiri kuhusu Ufalme na kufundisha “mambo yanayohusu Bwana Yesu Kristo.”—Mdo. 28:30, 31.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki