-
Kwa Nini Ponografia Imeenea Sana?Amkeni!—2003 | Julai 22
-
-
Madaktari fulani hudai kwamba ponografia inaweza kuanzisha zoea ambalo ni vigumu kuacha hata kuliko zoea la kutumia dawa za kulevya. Matibabu ya wale waliozoea dawa za kulevya mara nyingi huanza kwa kuondoa dawa hizo mwilini. Lakini zoea la ponografia, aeleza Dakt. Mary Anne Layden wa Chuo Kikuu cha Pennsylvania, “hutokeza picha akilini ambazo hudumu daima katika akili ya mtazamaji na kutia mizizi katika ubongo.” Ndiyo sababu watu wanaweza kukumbuka dhahiri picha za ponografia walizoona miaka iliyopita. Anamalizia kwa kusema: “Hii ndiyo kasumba ya kwanza ambayo haina tiba.”
-
-
Madhara Yanayosababishwa na PonografiaAmkeni!—2003 | Julai 22
-
-
Dakt. Victor Cline, mtaalamu wa kutibu watu wanaotawaliwa na mambo ya ngono, ametambua kwamba watu wanaotazama ponografia huendelea tu bila kuacha. Mtu anayeanza kutazama ponografia kidogo-kidogo, asipoacha mwishowe anaweza kuwa na zoea la kusoma habari na kutazama picha chafu zaidi za ponografia. Cline anadai kwamba zoea hilo linaweza kuongoza kwenye matendo mapotovu ya ngono. Wanasayansi wanaochunguza tabia za wanadamu wanakubaliana na jambo hilo. Dakt. Cline anaripoti kwamba “upotovu wowote wa ngono unaweza kuanza hivyo . . . na kwamba mtu hawezi kuacha hata akisumbuliwa sana na dhamiri.” Hatimaye, huenda mtu anayetazama ponografia akajaribu kufanya mambo yasiyo ya adili aliyoona, na mara nyingi matokeo huwa mabaya.
Tatizo hilo linaweza kuanza hatua kwa hatua bila kutambuliwa, asema Cline. Aongeza: “Huongezeka na kuenea kama kansa. Kwa kawaida zoea hilo halikomi, wala haliwezi kutatuliwa kwa urahisi. Haishangazi kwamba mara nyingi wanaume waliozoea kutazama ponografia hawakubali kwamba wana tatizo, na ni kawaida kwa wenzi wa ndoa kukosana, nyakati nyingine kutalikiana, na hata mahusiano mengine ya karibu huharibika kwa sababu hiyo.”
-