Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu
    Amkeni!—2007 | Machi
    • Watu wengi wanakubali kwamba simu za mkononi na Intaneti zina manufaa mengi. Hata hivyo, watu wengi huona kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Profesa Donald Roberts wa Chuo Kikuu anasema kwamba wanafunzi fulani “hawawezi kumaliza dakika chache za mapumziko bila kutumia simu zao za mkononi.” Anasema hivi: “Ni kana kwamba hawawezi kutulia hadi wazungumze kwenye simu, ni kama wanasema ‘mbona kuna kimya kingi sana.’”

      Vijana wengine wanakiri kwamba hawawezi kuishi bila vifaa hivyo. Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 16 aitwaye Stephanie anakiri hivi: “Mimi ni mraibu wa kutuma ujumbe wa haraka kupitia kompyuta na simu yangu ya mkononi, kwa sababu hiyo ndiyo njia kuu ya kuwasiliana na marafiki wangu. Ninaporudi nyumbani, mimi huenda moja kwa moja kwenye kompyuta na kutumia Intaneti mpaka saa tisa usiku.” Stephanie hulipa kati ya dola 100 hadi 500 kila mwezi kwa ajili ya gharama za simu. “Kufikia sasa, wazazi wangu wananidai zaidi ya dola 2,000 kwa sababu ya gharama za ziada za simu. Lakini nimezoea sana simu yangu ya mkononi hivi kwamba siwezi kufanya mambo yangu ya kawaida bila kuitumia.”

      Kuna matatizo mengine zaidi ya pesa zinazotumika. Alipokuwa anafanya utafiti kuhusu maisha ya familia, Elinor Ochs, mtaalamu wa tabia na tamaduni za wanadamu aligundua kwamba mzazi aliporudi nyumbani kutoka kazini, mara nyingi mwenzi wake wa ndoa na watoto walikuwa wakijishughulisha tu na kile walichokuwa wakifanya hivi kwamba mara 2 kati ya 3 hata hawakumsalimu! Waliendelea tu kukazia fikira vifaa vyao vya elektroniki. Ochs anasema, “Tuliona pia jinsi ilivyo vigumu kwa wazazi kujihusisha katika utendaji wa watoto wao.” Anaongezea kusema kwamba utafiti huo ulipokuwa ukiendelea, wazazi walionekana wakijaribu kuepuka kuwasumbua watoto ambao walikuwa wakikazia fikira mambo waliyokuwa wakifanya.

  • Kuwasaidia Vijana Wakabiliane na Hali Ngumu
    Amkeni!—2007 | Machi
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 6]

      Vituo vya Kuwasiliana—Simulizi la Msichana Mmoja

      “Nilianza kutumia kituo cha Intaneti cha shule yetu kuwasiliana na wanafunzi wenzangu na walimu. Nilianza kutumia saa moja kila juma kwenye kituo hicho. Baada ya muda nikaanza kukitumia kila siku. Nilikuwa nimenaswa sana hivi kwamba wakati ambapo sikuwa nikitumia Intaneti nilikuwa nikifikiria kuihusu. Sikuweza kukazia fikira kitu kingine chochote. Sikuweza kumaliza kazi yangu ya shuleni wala kukaza fikira nilipokuwa kwenye mikutano ya Kikristo, na hata niliwapuuza marafiki wangu. Mwishowe, wazazi wangu walitambua kilichokuwa kikiendelea nao wakaniwekea vizuizi. Ilikuwa vigumu kwangu kukubali vizuizi hivyo. Nilikasirika sana. Lakini sasa ninafurahi kwamba wazazi wangu walifanya hivyo nami nimefanya mabadiliko yanayofaa. Nisingependa kuhisi nimenaswa tena!”—Bianca.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki