Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • ‘Baba Yenu Ni Mwenye Rehema’
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • Kuwaonyesha Rehema Wakosaji

      8, 9. Rehema ambayo Daudi alionyeshwa baada ya dhambi yake pamoja na Bath-sheba ilitia ndani nini?

      8 Fikiria yale yaliyotukia baada ya nabii Nathani kuzungumza na Mfalme Daudi wa Israeli la kale kuhusu uzinzi wa Daudi pamoja na Bath-sheba. Daudi aliyetubu alisali hivi: “Ee Mungu, unionyeshe kibali kulingana na fadhili zako zenye upendo. Ufutilie mbali makosa yangu kulingana na wingi wa rehema zako. Unioshe kabisa kutokana na kosa langu, na kunitakasa kutokana na dhambi yangu. Kwa maana mimi mwenyewe nayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Dhidi yako wewe, wewe peke yako, nimetenda dhambi, nami nimefanya lililo baya machoni pako.”—Zaburi 51:1-4.

      9 Daudi alisikitika sana. Yehova alimsamehe dhambi yake na alijizuia kuwahukumu vikali Daudi na Bath-sheba. Kulingana na Sheria ya Musa, Daudi na Bath-sheba walipaswa kuuawa. (Kumbukumbu la Torati 22:22) Ingawa hawakuuawa, hawakuepuka matokeo mabaya ya dhambi yao. (2 Samweli 12:13) Rehema ya Mungu inatia ndani kusamehe makosa. Hata hivyo, hajizuii kutoa adhabu inayostahili.

  • ‘Baba Yenu Ni Mwenye Rehema’
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Septemba 15
    • 11. Yehova alionyesha jinsi gani kwamba hakupuuza haki aliposhughulikia dhambi ya Daudi pamoja na Bath-sheba?

      11 Daudi na Bath-sheba walipaswa kwanza kusamehewa kabla ya hukumu ya kifo kupunguzwa. Waamuzi wa Israeli hawakuruhusiwa kusamehe dhambi. Ikiwa wangeruhusiwa kushughulikia kisa hicho, wangelazimika tu kutoa hukumu ya kifo. Sheria ilitaka watoe hukumu hiyo. Hata hivyo, kwa sababu ya agano lake pamoja na Daudi, Yehova alitaka kuona ikiwa kulikuwa na msingi wa kusamehe dhambi ya Daudi. (2 Samweli 7:12-16) Hivyo, Yehova Mungu, yule “Mwamuzi wa dunia yote,” ambaye ni “mchunguzaji wa moyo,” aliamua kushughulikia kisa hicho yeye mwenyewe. (Mwanzo 18:25; 1 Mambo ya Nyakati 29:17) Mungu aliweza kusoma kwa usahihi moyo wa Daudi, akaona kwamba alikuwa ametubu kikweli, na hivyo akamsamehe.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki