Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutembea Kwenye Njia ya Watumwa
    Amkeni!—2011 | Mei
    • Kati ya karne ya 16 na 19, inakadiriwa kwamba Waafrika milioni 12 walisafirishwa kwa meli kupitia Bahari ya Atlantiki ili wakatumikishwe katika mashamba na migodi ya mabara ya Amerika. Kitabu American Slavery—1619-1877 kinasema kwamba asilimia 85 hivi ya watumwa hao “walipelekwa Brazili na huko Karibea katika nchi zilizokuwa koloni za Uingereza, Ufaransa, Hispania, na Uholanzi.” Asilimia 6 hivi walipelekwa kwenye koloni ambazo zingekuja kuwa sehemu ya Marekani.a

  • Kutembea Kwenye Njia ya Watumwa
    Amkeni!—2011 | Mei
    • Historia Ndefu Isiyopendeza

      Tangu hapo zamani, watawala Waafrika waliwauza mateka wao wa vita kwa Waarabu. Baadaye, nchi za Ulaya ziliingia kwenye biashara hiyo ya watumwa, hasa baada ya kupata koloni katika mabara ya Amerika. Wakati huo, vita vya kikabila na mateka waliochukuliwa walifanya kuwe na watumwa wengi, na hilo likafanya vita kuwa biashara yenye kuleta faida nyingi kwa washindi na pia kwa wafanyabiashara ya utumwa waliokuwa na pupa. Isitoshe, watumwa walitekwa nyara na wengine waliletwa na wafanyabiashara Waafrika kutoka sehemu za ndani za Afrika. Mtu yeyote angeweza kuuzwa kama mtumwa, hata mwana wa mfalme ambaye alikuwa amepoteza kibali cha mfalme.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki