Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Punde baadaye, ikaamuliwa gazeti la Mnara wa Mlinzi lichapishwe katika Kiafrikana. Ijapokuwa akina ndugu hawakujua wakati huo, ulikuwa uamuzi wa hekima kwa kuzingatia mambo yaliyotokea baadaye barani Ulaya. Mashini ya kupiga chapa na ya kukunja magazeti zikaanza kutumiwa. Toleo la kwanza lilitolewa Juni 1, 1940.

      Kufikia wakati huo, ndugu walikuwa wakipokea gazeti la Mnara wa Mlinzi la Kidachi kutoka Uholanzi kwa ajili ya wasomaji wa Kiafrikana, kwa kuwa lugha hizo mbili zinafanana. Lakini mwezi wa Mei 1940, kwa sababu Hitler alivamia Uholanzi, ofisi ya tawi ilifungwa ghafula. Hata hivyo, kwa kuwa tayari gazeti la Mnara wa Mlinzi lilikuwa limeanza kuchapwa katika Kiafrikana nchini Afrika Kusini, akina ndugu hawakukosa toleo lolote la gazeti hilo. Magazeti yaliyogawanywa kila mwezi yaliongezeka kufikia 17,000.

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MAENDELEO IJAPOKUWA VIKWAZO

      Kwa sababu ya uchochezi wa viongozi wa dini zinazodai kuwa za Kikristo na shuku ya serikali kufuatia msimamo wetu wa kutokuwamo, nakala za wale waliokuwa wameandikisha magazeti ya Mnara wa Mlinzi na Consolation zilitwaliwa mwaka wa 1940 na wenye mamlaka waliokuwa wameweka vikwazo. Tangazo rasmi la kupiga marufuku vichapo hivyo likatolewa. Magazeti na vitabu kutoka ng’ambo vilitwaliwa mara tu vilipowasili.

      Hata hivyo, bado akina ndugu walipokea chakula chao cha kiroho kwa wakati. Sikuzote, kwa njia moja au nyingine, ofisi ya tawi ilipata nakala ya Kiingereza ya gazeti la Mnara wa Mlinzi, kisha ikaitayarisha na kuichapa. George Phillips aliandika hivi: “Wakati wa marufuku, tulijionea . . . mambo mengi yenye kupendeza yaliyotuthibitishia kwamba Yehova alikuwa akiwatunza na kuwalinda watu wake kwa upendo. Hatukukosa hata toleo moja la Mnara wa Mlinzi. Mara nyingi tulipokea nakala moja tu. Nyakati fulani tungepata tulichohitaji kutoka kwa mwandikishaji aliyekuwa katika mojawapo ya nchi za Rhodesia [ambazo leo zinaitwa Zambia na Zimbabwe] au kutoka katika eneo la Afrika Mashariki lililokuwa likitawaliwa na Wareno [ambalo leo linaitwa Msumbiji] au mashambani nchini Afrika Kusini au kutoka kwa mgeni aliyekuwa akisafiri kwa mashua ambayo ilitia nanga Cape Town.”

  • Afrika Kusini
    2007 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 87]

      Magazeti ya “Consolation” na “Mnara wa Mlinzi” ya kwanza kuchapishwa katika Kiafrikana

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki