-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na yeye akafungua shimo la abiso, na moshi ukapaa kutoka shimo kama moshi wa tanuri kubwa, na jua likatiwa giza, pia hewa, kwa moshi wa shimo lile.
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
8. Inakuwaje kwamba kuachiliwa kwa wale nzige kunaandamana na “moshi” mwingi?
8 Yohana anapotazama, kuachiliwa kwa nzige kunaandamana na moshi mwingi, kama “moshi wa tanuri kubwa.”c Ndivyo ilivyothibitika kuwa katika 1919. Hali ilikuwa yenye giza kwa Jumuiya ya Wakristo na kwa ulimwengu kwa ujumla. (Linga Yoeli 2:30, 31.) Kuachiliwa kwa hao nzige wa jamii ya Yohana kulikuwa ushinde kikweli kwa viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo, ambao walikuwa wametunga hila ya kuua kabisa kazi ya Ufalme na ambao sasa walikataa Ufalme wa Mungu. Ithibati ya giza lenye kufunika kama moshi ilianza kuenea juu ya Jumuiya ya Wakristo yenye kuasi imani wakati hicho kikosi cha nzige kilipopewa mamlaka na kikaanza kuitumia katika kupiga mbiu ya jumbe za hukumu zenye kujaa nguvu. “Jua” la Jumuiya ya Wakristo mwonekano wayo wa kuwa mtio-nuru—lilipatwa na giza, na “hewa” ikawa nzito kwa majulisho-wazi ya hukumu za kimungu wakati “mtawala wa mamlaka ya hewa” alipoonyeshwa kuwa ndiye mungu wa Jumuiya ya Wakristo.—Waefeso 2:2, NW; Yohana 12:31; 1 Yohana 5:19.
-
-
Ole wa Kwanza—NzigeUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
c Angalia kwamba andiko hili haliwezi kutumiwa kuthibitisha kwamba ndani ya abiso ulikuwamo moto, kana kwamba abiso ilikuwa namna fulani ya moto wa mateso. Yohana anasema yeye aliona moshi mzito uliokuwa “kama,” au mfano wa moshi wa tanuri kubwa. (Ufunuo 9:2) Yeye haripoti kuwa anaona miale hasa katika abiso.
-