-
Wenye Furaha Ni Yule Ambaye Mungu Wake Ni YehovaMnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 26]
Jumba la Ufalme la kwanza huko Anchorage
-
-
Wenye Furaha Ni Yule Ambaye Mungu Wake Ni YehovaMnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 1
-
-
Yehova Aukuza Ukweli Huko Alaska
Ziara yangu ya kwanza huko Fairbanks ilikuwa yenye kutia moyo sana. Tulipata matokeo mazuri katika huduma, na karibu watu 50 walihudhuria hotuba ya watu wote Jumapili hiyo. Tulikutana katika makao madogo ya mishonari walikoishi Vernor na Lorraine Davis. Watu walikuwa wakichungulia kutoka jikoni, chumba cha kulala, na ukumbini ili kusikia hotuba. Kwa kuwa watu wengi walikuja kusikia hotuba hiyo, tulijua kwamba ikiwa Jumba la Ufalme lingejengwa mahali hapo, kazi ya kuhubiri ingeimarika huko Fairbanks. Kwa hiyo, kwa msaada wa Yehova, tulinunua nyumba kubwa kiasi iliyotumiwa kama ukumbi wa kuchezea dansi na kuihamisha hadi kwenye kiwanja kinachofaa. Tulichimba kisima, tukajenga vyoo, na kuweka mfumo wa kupasha jumba joto. Katika muda wa mwaka mmoja, Jumba la Ufalme lilianza kutumiwa huko Fairbanks. Baada ya kujenga jikoni, jumba hilo lilitumiwa kwa ajili ya kusanyiko la wilaya mwaka wa 1958, na watu 330 walihudhuria.
-
-
Wenye Furaha Ni Yule Ambaye Mungu Wake Ni YehovaMnara wa Mlinzi—2003 | Agosti 1
-
-
Majumba mapya ya Ufalme yalijengwa huko Juneau na Whitehorse, Yukon, na vikundi vipya kadhaa vilivyojitenga vikaanzishwa.
-