Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • John Marks, aliyezaliwa kusini mwa Albania, ambaye alikuwa akiishi Marekani, aliombwa ajaribu kupata kibali cha kuingia Albania.

      Mwaka mmoja na nusu baadaye, John alifanikiwa kupata kibali, ingawa mke wake Helen hakupata. John alifika Durrës Februari 1961 na kusafiri hadi Tiranë. Alikutana na dada yake, Melpo, aliyekuwa ameanza kupendezwa na kweli. Melpo alimsaidia kukutana na akina ndugu siku iliyofuata.

      John aliongea na ndugu hao kwa muda mrefu kisha akawapa vitabu na magazeti kadhaa aliyokuwa ameficha katika sanduku lake. Ndugu hao walisisimuka. Hawakuwa wametembelewa na ndugu kutoka nje ya Albania kwa zaidi ya miaka 24.

      Kulingana na John, kulikuwa na ndugu 60 katika miji mitano na wengine wachache katika vijiji vidogo-vidogo. Mjini Tiranë, ndugu walijaribu kukutana kisiri mara moja kwa juma, siku ya Jumapili, ili kusoma pamoja vitabu walivyokuwa wameficha tangu 1938.

      Kwa kuwa kwa muda mrefu mawasiliano kati yao na tengenezo yalikuwa yamekatizwa, ndugu hao wa Albania walihitaji kufahamishwa mambo ya kitengenezo na kweli za karibuni. Kwa mfano, akina ndugu na dada walikuwa wakiongoza mikutano na hata akina dada walikuwa wakitoa sala. Baadaye John aliandika: “Akina ndugu hawakujua jinsi dada hao wangeitikia, hivyo wakaniomba nizungumze nao faraghani, nami nikafanya hivyo. Nafurahi kwamba waliyakubali marekebisho hayo.”

      Licha ya umaskini wao, watumishi hao waaminifu waliunga mkono kazi ya Ufalme kwa bidii. Kwa mfano, John anakumbuka ndugu wawili waliokuwa wazee kwa umri kutoka Gjirokastër ambao walikuwa wameweka akiba “kutokana na pesa kidogo walizokuwa nazo, nao walikuwa wamekusanya kiasi walichotaka kutoa kiwe mchango kwa Sosaiti.” Kila mmoja wao alikuwa amehifadhi zaidi ya sarafu za dhahabu zenye thamani ya dola 100.

      Ndugu wa Tiranë walithamini kupokea kijitabu Preaching and Teaching in Peace and Unity, kilichotoa mwongozo kuhusu jinsi makutaniko yanapaswa kutenda, hata chini ya marufuku. Kisha, mnamo Machi, John akafanya Ukumbusho huko Tiranë nyumbani kwa Leonidha Pope, kukiwa na hudhurio la watu 37. Baada ya hotuba hiyo, John akapanda mashua na kurudi Ugiriki.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 149]

      Helen na John Marks kabla ya John kurudi Albania

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki