Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Baada ya ndugu katika makao makuu kusoma ripoti ya John kuhusu ziara yake nchini Albania, walimweka Leonidha Pope, Sotir Papa, na Luçi Xheka kusimamia Kutaniko la Tiranë na vilevile kazi nchini Albania.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • MWANZO MZURI—KISHA MATATIZO

      Ingawa Halmashauri ya Nchi ilijitahidi kuendeleza ibada safi, matatizo yalikuwa njiani. Mwaka wa 1963, Melpo Marks alimwandikia John, ndugu yake, kwamba ndugu wawili wa Halmashauri ya Nchi, Leonidha Pope na Luçi Xheka, hawakuwa “pamoja na familia zao” na kwamba mikutano haifanywi. Baadaye kukawa na fununu kwamba Spiro Vruho yuko hospitalini, naye Leonidha Pope na Luçi Xheka ni wagonjwa, andiko la Matendo 8:1, 3 lilirejelewa, ambapo Sauli wa Tarso aliwatia Wakristo gerezani. Ni nini kilichokuwa kikiendelea?

      Leonidha Pope, Luçi Xheka, na Sotir Ceqi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda fulani ambapo washiriki wa Chama cha Kikomunisti walifanya mkutano na wafanyakazi wote, wakipigia debe dhana za Kikomunisti. Siku moja, kulipokuwa na mazungumzo kuhusu mageuzi, Leonidha na Luçi walisimama na kusema: “Hapana! Mwanadamu hakutokana na nyani!” Siku iliyofuata walichukuliwa na kutenganishwa na familia zao, na kupelekwa kufanya kazi uhamishoni katika miji ya mbali, adhabu ambayo huitwa internim (korokoroni) na Waalbania. Luçi alipelekwa katika milima ya Gramsh.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Kufikia Agosti 1964, karibu mikutano yote iliacha kufanywa. Ripoti chache zilizopokewa zilionyesha kwamba ndugu hao walikuwa chini ya uchunguzi mkali wa Sigurimi. Stempu moja ilikuwa na ujumbe huu: “Mwombeni Bwana kwa niaba yetu. Nyumba zinapekuliwa. Hawaturuhusu kujifunza. Watatu wako korokoroni.” Mwanzoni, ilidhaniwa kwamba ndugu Pope na Xheka walikuwa wameachiliwa, kwa kuwa wao tu ndio waliojua mbinu hiyo ya kuandika chini ya stempu. Hata hivyo, baadaye ilikuja kujulikana kwamba Frosina, mke wa Luçi, ndiye aliyekuwa ametuma ujumbe huo.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 151, 152]

      “Yehova Hakutuacha Kamwe!”

      FROSINA XHEKA

      ALIZALIWA 1926

      ALIBATIZWA 1946

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Alijifunza kweli alipokuwa kijana. Ijapokuwa wazazi wake walimpinga, na wenye mamlaka wakamtenga na wengine, sikuzote alihisi akiwa karibu na Yehova na tengenezo lake. Alikufa akiwa mwaminifu mwaka wa 2007.

      ◼ FROSINA alijifunza kweli kutoka kwa ndugu zake katika miaka ya 1940. Wazazi wake ambao hawakuwa Mashahidi walimfukuza nyumbani kwa sababu alikataa kuolewa na mwanamume waliyemchagulia. Familia ya ndugu mmoja, Gole Flloko, ilimchukua na kukaa naye kama binti yao.

      “Pindi moja nilikamatwa kwa sababu ya kukataa kupiga kura,” asema Frosina. “Nilikuwa peke yangu katika chumba. Ghafula nikazingirwa na maofisa 30 hivi. Mmoja wao akasema kwa sauti kubwa, ‘Unajua tunaweza kukufanya nini?’ Nilihisi kwamba Yehova yu nami na kusema, ‘Hamwezi kufanya lolote ambalo Bwana Mwenye Enzi Kuu Yehova hatawaruhusu mfanye!’ Walidhani nina wazimu, wakaniambia, ‘Ondoka!’ Waona, sikukosea. Yehova alikuwa nami!”

      Mwaka wa 1957, Frosina aliolewa na Luçi Xheka, na hatimaye wakawa na watoto watatu. Mapema miaka ya 1960, Luçi aliwekwa kuwa mshiriki wa Halmashauri ya Nchi, iliyokuwa imeundwa ili kusimamia kazi nchini Albania. Muda si muda akahukumiwa kifungo cha miaka mitano huko Gramsh, mbali na Frosina na watoto wake. Akiwa huko, Luçi aliendelea kuhubiri na kuzungumza kuhusu tengenezo la Yehova. Watu wa Gramsh wanamkumbuka hadi leo hii.

      Luçi alipokuwa kifungoni, Chama cha Kikomunisti kiliweka jina la Frosina katika orodha ya washukiwa, na kwa sababu hiyo asingeweza kununua chakula. Frosina anasema: “Haikudhuru. Ndugu wachache waliokuwapo walinigawia chakula chao! Tulisonga mbele kwa kuwa Yehova hakutuacha kamwe!”

      Luçi alipokufa, ikawa vigumu kukutana na akina ndugu. Hata hivyo, Frosina aliendelea kuhubiri. Anakumbuka: “John Marks alitutembelea miaka ya 1960. Hatimaye nilipokutana na mke wake, Helen, mwaka wa 1986, ni kana kwamba tulikuwa tumejuana kwa muda mrefu. Luçi nami tulikuwa tukiwatumia akina Marks ujumbe kisiri, nao wakawa wakiwatumia ndugu huko Brooklyn.”

      Marufuku ilipoondolewa mwaka wa 1992, Frosina alikuwa mmoja wa Mashahidi tisa waliobatizwa ambao walikuwa wamebaki Albania. Alikuwa wa kawaida katika mikutano naye alikuwa shambani siku aliyokufa mwaka wa 2007. Muda mfupi kabla hajafa, Frosina alisema: “Nampenda Yehova kwa moyo wangu wote! Sijawahi kamwe kufikiria kuridhiana imani yangu. Nilijua kwamba nina familia kubwa ulimwenguni pote, lakini sasa siamini ninapoona jinsi familia yetu ya kitheokrasi ilivyo kubwa hapa Albania. Yehova amekuwa nasi sikuzote, nasi tungali katika mikono yake yenye upendo!”

      [Picha]

      Frosina Xheka mwaka wa 2007

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki