-
Albania2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Leonidha Pope, Luçi Xheka, na Sotir Ceqi walikuwa wakifanya kazi katika kiwanda fulani ambapo washiriki wa Chama cha Kikomunisti walifanya mkutano na wafanyakazi wote, wakipigia debe dhana za Kikomunisti. Siku moja, kulipokuwa na mazungumzo kuhusu mageuzi, Leonidha na Luçi walisimama na kusema: “Hapana! Mwanadamu hakutokana na nyani!” Siku iliyofuata walichukuliwa na kutenganishwa na familia zao, na kupelekwa kufanya kazi uhamishoni katika miji ya mbali, adhabu ambayo huitwa internim (korokoroni) na Waalbania. Luçi alipelekwa katika milima ya Gramsh.
-
-
Albania2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Hata hivyo, ndugu waliokuwa korokoroni waliwatolea ushahidi mzuri mtu yeyote waliyekutana naye. Watu wa Gramsh walikuwa wakisema: “Ungjillorë [wainjilisti] wako hapa. Hawajiungi na jeshi, lakini wanatujengea madaraja na kurekebisha majenereta.” Sifa nzuri ya ndugu hao ilijulikana kwa miaka mingi.
-