-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Baadaye nilirudi Mbreshtan ili kufuatia kazi yangu ya ushonaji wa viatu.
-
-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Kurudi Kijijini Kwetu
Katika 1947 familia yangu nami tukarudi Mbreshtan. Muda mfupi baadaye, katika alasiri moja ya Desemba yenye ubaridi sana, niliitwa ofisini mwa Sigurimi (polisi wa siri). “Je, wajua ni kwa nini nimekuita?” huyo ofisa akauliza.
“Nawazia ni kwa sababu umesikia mashtaka dhidi yangu,” nikajibu. “Lakini Biblia husema kwamba ulimwengu ungetuchukia, kwa hiyo mashtaka hayanishangazi.”—Yohana 15:18, 19.
“Usiongee juu ya Biblia nami,” akaitikia kwa ukali. “Nitakupiga vibaya sana.”
Huyo ofisa na watu wake wakaondoka lakini wakaniamuru nisimame nje katika baridi. Baada ya muda fulani akaniita tena ofisini mwake na kuniamuru niache kufanya mikutano nyumbani kwetu. “Ni wangapi wanaoishi kijijini mwako?” yeye akauliza.
“[Watu] mia na ishirini,” nikasema.
“Wao ni wa dini gani?”
“Othodoksi ya Kialbania.”
“Na wewe?”
“Mimi ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova.”
“Watu mia moja na ishirini hufuata njia moja na wewe hufuata nyingineyo?” Kisha akaniamuru niwashe mishumaa kanisani. Nilipomwambia kuwa nisingefanya hivyo, akaanza kunipiga kwa ufito. Ilikuwa karibu saa saba usiku nilipoachiliwa hatimaye.
-