Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • John alifika Durrës Februari 1961 na kusafiri hadi Tiranë. Alikutana na dada yake, Melpo, aliyekuwa ameanza kupendezwa na kweli. Melpo alimsaidia kukutana na akina ndugu siku iliyofuata.

      John aliongea na ndugu hao kwa muda mrefu kisha akawapa vitabu na magazeti kadhaa aliyokuwa ameficha katika sanduku lake. Ndugu hao walisisimuka. Hawakuwa wametembelewa na ndugu kutoka nje ya Albania kwa zaidi ya miaka 24.

      Kulingana na John, kulikuwa na ndugu 60 katika miji mitano na wengine wachache katika vijiji vidogo-vidogo. Mjini Tiranë, ndugu walijaribu kukutana kisiri mara moja kwa juma, siku ya Jumapili, ili kusoma pamoja vitabu walivyokuwa wameficha tangu 1938.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu wa Tiranë walithamini kupokea kijitabu Preaching and Teaching in Peace and Unity, kilichotoa mwongozo kuhusu jinsi makutaniko yanapaswa kutenda, hata chini ya marufuku. Kisha, mnamo Machi, John akafanya Ukumbusho huko Tiranë nyumbani kwa Leonidha Pope, kukiwa na hudhurio la watu 37. Baada ya hotuba hiyo, John akapanda mashua na kurudi Ugiriki.

      Baada ya ndugu katika makao makuu kusoma ripoti ya John kuhusu ziara yake nchini Albania, walimweka Leonidha Pope, Sotir Papa, na Luçi Xheka kusimamia Kutaniko la Tiranë na vilevile kazi nchini Albania.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki