-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
jiji la Tiranë, jiji kuu la Albania. Nikiwa huko nilikutana na Stathi Muçi, aliyekuwa akisoma Biblia ya Kigiriki. “Je, wewe huenda kanisani?” nikauliza. “La,” yeye akajibu. “Nililiacha kanisa. Mimi ni mmoja wa Wanafunzi wa Biblia wa Kimataifa.” Jumapili, askari-jeshi mwingine nami tukaenda kwenye mkutano pamoja na Stathi. Huko nilijifunza kwamba kanisa la kweli si jengo wala dini fulani, bali limefanyizwa na watumishi watiwa-mafuta wa Kristo. Sasa nikaelewa kile ambacho kitabu The Harp of God kilikuwa kikisema.
Nasho Idrizi na Spiro Vruho walikuwa wamerudi Albania kutoka Marekani katika miaka ya katikati ya 1920 nao walikuwa wakieneza kweli za Biblia ambazo walikuwa wamejifunza huko. Nilianza kuhudhuria mikutano katika Tiranë, pamoja na wale Wanafunzi wa Biblia wachache. Upesi ikawa wazi kwangu kwamba nilikuwa nimelipata tengenezo la Yehova. Kwa hiyo mnamo Agosti 4, 1930, nilibatizwa katika mto wa karibu.
-
-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Tulimaliza ziara hiyo katika Tiranë wakati barabara ili kuadhimisha Ukumbusho wa kifo cha Kristo.
-
-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Miezi mitatu baadaye tulihamishwa hadi gereza lililoko Tiranë na kufungwa kwa miezi mingine minane bila kuhukumiwa.
Hatimaye, tulipelekwa mbele ya mahakama ya kijeshi. Ndugu Shyti nami tulihukumiwa kifungo cha miezi 27, Ndugu Komino miezi 24, na wale wengine waliachiliwa huru baada ya miezi 10.
-
-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Mashahidi katika Tiranë wakashikwa, na watatu wakapewa kifungo cha miaka mitano katika kambi ya kufanyia kazi nzito iliyokuwa mbali. Likiwa tokeo, familia zao ziliteseka.
-
-
Yehova Hakutuacha KamweMnara wa Mlinzi—1996 | Januari 1
-
-
Katika 1975, Argjiro nami tulikaa na mwana wetu katika Tiranë kwa miezi michache. Wakati wa uchaguzi, wenye mamlaka jijini walituwekea mkazo kwa kututisha hivi: “Msipopiga kura, tutamnyang’anya mwana wenu kazi yake.”
“Mwanangu amekuwa akifanya kazi kwa miaka 25,” nikajibu. “Nyinyi mna rekodi za kibinafsi zenye mambo mengi juu yake na familia yake. Mimi sijapiga kura kwa zaidi ya miaka 40. Kwa kawaida habari hiyo huwa katika rekodi za wafanyakazi. Ikiwa haimo, basi rekodi zenu zina kasoro. Ikiwa imo katika rekodi zenu, basi hamjawa waaminifu-washikamanifu kwa chama kwa kumruhusu afanye kazi kwa miaka mingi hivyo.” Waliposikia hilo, wenye mamlaka wakasema kwamba ikiwa tungerudi Mbreshtan, wao wasingesisitiza juu ya jambo hilo.
-