Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • HALI ZAANZA KUBADILIKA

      Hali ya kisiasa ilianza kubadilika mwaka wa 1989. Hukumu ya kifo kwa wanaojaribu kutoroka Albania ilifutiliwa mbali.

  • Albania
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ukuta wa Berlin ulibomolewa Novemba 9, 1989, na punde baadaye matokeo yake yakaanza kuonekana nchini Albania. Machi 1990 ghasia dhidi ya Ukomunisti zilizuka huko Kavajë. Maelfu ya watu walimiminika katika ofisi za ubalozi za nchi za kigeni mjini Tiranë wakitaka kuondoka nchini. Wanafunzi walidai mabadiliko nao wakagoma kula.

      Februari 1991, umati mkubwa wa watu ukaiangusha sanamu ya Enver Hoxha, yenye urefu wa mita 10, iliyokuwa kwa miaka mingi katika Bustani ya Skanderbej huko Tiranë. Kulingana na watu hao, dikteta huyo hakuwapo tena. Mwezi wa Machi, Waalbania 30,000 hivi waliteka nyara meli kadhaa kutoka Durrës na Vlorë na kusafiri hadi Italia wakiwa wakimbizi. Mwezi huohuo, uchaguzi wa vyama vingi ulifanywa kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi. Ingawa Chama cha Kikomunisti kilishinda uchaguzi huo, ni wazi kwamba serikali ilikuwa imedhoofika.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki